Tangu Zama za kale Jamii Mbalimbali zilijiwekea utaratibu Wa kuhesabu Watu wake ili kubaini Idadi Yao na kuweza kuwapatia Mahitaji Yao ya Msingi na kugawanya Rasilimali za Jamii kwa Usawa. Hata moja ya Vitabu vya iman imeeleza Namna Jamii ya Watu Wa walivyo weza kutekeleza zoezi la kuhesabiana ili kutambuana Kichwa kwa Kichwa Nyumba kwa Nyumba,ili Kuwa watambua Jamii ya ile Baada ya kutoka uhamishoni Misri. Uthibitisho wa Jambo Hili unaweza soma Katika Biblia Katika kitabu Cha Hesabu 1:2-3 Tanzania ikiwa Miongoni mwa Jamii iliyo Chini ya Dunia nayo imefuata utaratibu huu wa kuhesabiana Kama ilivyo fanyika hata Katika Jamii za kale Tangu Zama za Kale. Sensa si zoezi geni hapa nchini Tanzania Kwani Miaka kadhaa iliyopita limefanyika, sensa ya kwanza ikiwa Ni Mwaka 1967, nakufuatiwa nazoezi la Sensa nyingine Kati ya mwaka 1978,1988, 2002 Na sensa ya Mwisho ilifanyika Agost, 2012. Sensa itakayo fanyika Mapema Agosti 23,2022 itakua Ni sensa ya Sita Tangu Tanzan...