RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo kwa kutekeleza vema majukumu yake katika kipindi chake chote cha utumishi ndani ya Jeshi hilo.
Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo alipozungumza na Jenerali Mabeyo ambaye alifika Ikulu Zanzibar kumuaga Rais kufuatia kumaliza muda wa utumishi wake ndani ya Jeshi mwisho wa mwezi wa sita kwa mujibu wa sheria.
Jenerali Mabeyo alisema Jeshi la Ulinzi Tanzania litaendelea kumkumbuka Rais Dk. Mwinyi kwa busara na hekima zake katika kuzishughulikia changamoto mbalimbali ndani ya Jeshi hilo ambalo hatimae limepata mafanikio makubwa.
📆 06 Juni, 2022
Ikulu,Zanzibar
#Lucas Ambrose Mboje
Comments
Post a Comment