Katika kuhakikisha Serikali inaleta unafuu wa Maisha Kwa Wananchi wake Pamoja na kudhibiti mfumuko wa Bei za Bidhaa na huduma nchini,Serikali inatarajia kupunguza ushuru wa Forodha Kwa Bidhaa za Mafuta ya Petroli nchini.
Hayo Yamesemwa Mapema Jana na Waziri wa Fedha na Mipango,Mhe.Mwigulu Lameck Nchemba Wakati Wa Uwasilishaji wa hotuba ya Bajeti Ya mapato na matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/23,Bungeni Dodoma Juni 14,2022.
Waziri Mwigulu Ameeleza kuwa Uamizi huu umefikiwa na Nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki,Ambapo Ushuru wa Forodha kwa Nchi wanachama utashuka Kutoka asilimia 25 Ya Sasa Hadi kufikia asilimia 10 kwa Mwaka wa Fedha 2022/23. Hii imelenga kutoa unafuu na kuwalinda watumiaji wa Bidhaa za Mafuta ya Petroli.
"Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwenye mafuta mengineyo ya petroli yanayotambulika kwa HS Code 2710.19.10. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu na kulinda watumiaji wa bidhaa hii" Alieleza Waziri Mwigulu.
Bei ya Bidhaa ya Mafuta ya petrol Katika Siku za karibuni zimezidi kupaa,Hali hii Ikisababishwa na madhara ya UVIKO 19 na Vita Kati ya Urusi na Ukraine,Sababu hii imepelekea Gharama za Maisha kupanda na mfumuko wa Bei za Bidhaa na huduma Duniani Kote,Huku hali Ikiwa Mbaya Zaidi katika nchi zinazo endelea.
📸 @mofURT
Comments
Post a Comment