Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hasani,Ameipongeza timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 17 Serengeti Girls Kwa Kufuzu kushiriki mashindano ya kombe la Dunia wanawake chini ya miaka 17 Yanayotarajia Kufanyika nchini India Mwezi Oktoba.
Mhe.Rais Samia kupitia ukarasa wake wa mtandao wa twita ameandika "Nawapa Pongezi Timu ya Taifa ya Soka la Wanawake chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2022. Hongera kwa benchi la ufundi na wote waliochangia kufikia hatua hii. Mmeweka historia kubwa na adhimu kwa nchi yetu. Ninyi ni fahari ya Watanzania".
Kwa Upande mwingine Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa akiwa bungeni Mapema leo Juni 6,2022 Ameipongeza timu Hiyo ya wanawake na amewapongeza wanawake wote nchini Kwa heshima wanayo endelea kuiletea Nchi Yetu katika nyanja mbalimbali.
"Hongereni Sana Serengeti Girls, Hongera Sana Mhe. Rais, Hongereni sana Wanawake wote wa Tanzania, hakika mmetuheshimisha,.."
Timu ya wanawake(Serengeti Girls) chini ya miaka 17 ilipata ushindi wa Jumla ya magoli 5-1 dhidi ya timu Ngumu ya Cameruni hapo jana,Ambapo katika mchezo wa awali uliochezwa nchini Cameruni walishinda kwa magoli 4-1 na mchezo wa marudiano ulimalizika kwa Ushindi wa Goli 1-0, Hivyo Serengeti Girls Kufuzu kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia kwa Mara ya kwanza,Yanayotarajia Kufanyika nchini India Mwezi Oktoba,2022.
Comments
Post a Comment