Na.Anthonius Kuzenza
Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hasani, Amewaasa makatibu Mahsusi watunza kumbukukumbu,Pamoja na Maafisa utumishi kutunza Siri Za Seikali.
Wito Huo umetolewa leo Juni2,2022 wakati Wa ufunguzi wa Mkutano wakitaaluma wa Chama Cha Makatibu mahususi (TAPSEA) Uliofanyika Leo katika Ukumbi wa Mkutano JKCC jijini Dodoma.
Raisi Samia amesisitza kuwa Suala la utumzaji wa Siri za serikali linaepusha madhara mbali mbali kwa Taasisi,Mtu binafsi na Usalama wa Taifa kwa ujumla.
Raisi Ameongeza kuwa uzalendo, uadilifu na weledi vyote hivi vinaweza kuwa njia ya kuwafanya Makatibu Mahsusi kuaminiwa na kutegemewa na kupelekea kusonga Mbele katikaa utumishi wao wa Kila siku.
Katika hatua nyingine Raisi Samia Suluhu Hasani ameridhia Chuo Cha Utumishi wa umma Tabora kiwe mahususi kwa kutoa mafunzo ya Uhazili kwa ngazi zote ili kuzalisha wataalam katika Taaluma ya Ukatibu Mahsusi watakao tumika katika Taasisi za serikali kote nchini.
Raisi Samia Amesema Serikali inaendelea kuimarisha mifumo ya kiutumishi pamoja na kuboresha maslahi kwa watumishi wa umma.
Picha na @ikulumawasliano
Comments
Post a Comment