Picha na East African Television(EATV)
Na Anthonius-Kuzenza
Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Mwigulu Lameck Nchemba Amewapongeza wanawake wote nchini kwa Uaminifu wao katika kurejesha Mikopo.
Waziri Dk.Mwigulu Aliyasema Hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Makadilio ya Bajeti kuu ya Serikali mapema mwanzoni mwa Juma Hili Juni 14,2022.
"Niwapongeze sana
wanawake, taarifa za kitafiti nilizopewa
zinaonesha wanawake wengi wanajitahidi
kurejesha mikopo kwa uaminifu"
Aidha Dk.Mwigulu Aliongeza pia Mikopo inayokopwa na wanawake Maranyingi hutumika kwa kazi iliyokisudiwa, Ikilinganishwa na Ile Mikopo inayochukuliwa na Wanaume, Ambao urejeshaji wa Mikopo kwa wanaume Huwa unasuasua Ikilinganishwa na Wanawake.
"Hata mikopo ya familia kama imekopwa na wanawake, mingi huwa inafanya kazi iliyokusudiwa na hivyo inarejeshwa kwa uaminifu kuliko iliyokopwa na wanaume wengi ambao huwa hawarejeshi"
Hata hivyo Dk.Mwigulu Ametoa wito kwa Watu Wote kujenga utamaduni wa kukopa fadha kwa kuzingatia Kanuni,Na uwezo wa kurejesha mikopo ili kuweza kuinua Uchumi wa mtu mmoja mmoja na Nchi kwa ujumla.
Serikali Imekusudia kuendelea kutoa Mikopo kwa wafanyabiashara wadogo kwa Wakubwa katika mwaka wa Fedha 2022/23, huku ikiendelea kuweka Mazingira wezeshi ya mikopo Kwa lengo la kuchochea ukuaji wa Uchumi Kwa Mtu mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla.
Comments
Post a Comment