Na.Anthonius Kuzenza- Kigoma
Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na maji (EWURA) imetangaza Bei za ukomo kwa bidhaa za mafuta ya petrol,dizeli na mafuta ya Taa,zinazo Anza kutumikia leo Jumatano Juni 1,2022.
Kushuka kwa bei kumesababishwa na Ruzuku ya Tsh. Bilioni 100 iliyowekwa na serikali ya awamu ya sita Chini ya Mh. Raisi Samia Suluhu Hasan Ili Kukabiliana na mfumuko wa Bei ya Bidhaa za petrol na kuleta Ahueni kwa Wananchi.
Kufuatia Kutolewa KWA Ruzuku Kumepelekea Bei ya mafuta ya Petrol kushuka kwa Tsh.306 kwa Lita moja na Tsh.320 KWA kila Lita ya mafuta ya Dizeli, katika Bandari ya Dar-es-salaam.
Kwa Mkoa Wa Kigoma baada ya Serikali Kuweka Ruzuku Bei Petroli ina kuwa Kama ifuatavyo Wilaya ya Kigoma mjini Tsh.3156 Uvinza Tsh.3147 ,Buhigwe 3154,Kakonko 3156, Kasulu 3165 na kibondo 3163.
Kwa upande Wa Dizeli Bei zitakazo tumika Wilaya ya Kigoma mjini Tsh. 3293,Uvinza Tsh.3283, Buhigwe 3291, Kakonko 3293, Kasulu 3302 na kibondo 3300.
Aidha Bei ya mafuta ya Taa Wilaya ya Kigoma mjini Tsh. 3462,Uvinza Tsh.3452, Buhigwe 3459, Kakonko 3461, Kasulu 3471 na kibondo 3468.
Mamlaka imewataka Wauzaji wa Jumla wa bidhaa za petrol Nchini, kuuza bidhaa kwa Bei elekezi iliyo elekezwa na serikali,Ili kuepuka Hatua za kisheria zitakazo chukuliwa pindi wakikiuka maelekezo Hayo.
Comments
Post a Comment