Na.Anthonius Kuzenza.
Serikali Kupitia Wizara ya Maliasili Na utalii imetangaza Ruhusa ya Usafirishaji wa Wayamapori hai Kwenda nje Ya Nchi mapema Leo Juni4,2022 Ikiwa Ni baada ya katazo la Serikali la mwaka 2016.
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori iliyotolewa mapema leo, Serikali imetangaza kuwa Ruhusa hiyo itadumu kwa Kipindi Cha miezi 6 na hiyo itaanza kutumika Rasmi mapema Juni 6,2022 Hadi Disemba 5,2022.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Wanyama wanaohusika ni wale waliokuwa wamesalia kwenye mazizi na mashamba Baada ya zuio la hapo awali 2016.
Aidha Serikali imewataka Wafanya Biashara Wenye Wanyamapori na walio hakikiwa, Ikiwa Ni pamoja na Wenye Leseni za Biashara ya Nyara zilizo huishwa kisheria Kuwasilisha Nyaraka Hizo Ofisi za Utalii na Huduma za Biashara za jijini Arusha na Dar-es-Salaam.
Pia taarifa hiyo imeainisha kuwa Usafirishaji wote wa Wanyamapori utafanyika kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) imehitimisha Taarifa.
Comments
Post a Comment