picha chanzo @SimbaSCTanzania
Na.Anthonius Kuzenza
Timu za soka nchini Tanzania Simba na Yanga Zenye Maskani yake Jijini Dar mitaa ya Kariakoo Msimbazi na Jangwani,Zimezindua kampeni maalum Ijulikanayo Kama *_Nani zaidi_* Yenye lengo La kuimarisha na kujenga Uwezo wa kiuchumi kwa Klabu Zote Mbili, kwa kuwahusisha wapenzi na mashabiki Wa Timu hizo pendwa nchini Kupitia kupiga kura Huku wakichangia Kiasi Cha Tsh.1000 kwa kura Moja
Wakizungumza Mapema leo Juni 2,2022, Kupitia Vyombo vya Habari Viongozi wa Timu Zote Mbili Wamesema kampeni hii imekuja Muda Muafaka kwani Timu Hizi pacha zimekua Ni za Muda mrefu lakini hazijafikia mafanikio Makubwa yenye kuonekana yani kiuchumi na hata miundo mbinu licha ya mtaji wa kujizolea wapenzi na mashabiki Lukuki ndani na nje ya Nchi.Hivyo Kampeni hii itatumiwa na timu Zote kwa kuwahusisha mashabiki na wapenzi Kupiga kura Huku wakichangia Timu Zao Ili kuziwezesha kujimarisha kiuchumi.
Kampeni hii inayo simamiwa na Azam Tv Pamoja Azam pay Pamoja na Kampuni ya Agranfore, inalenga Kizishindanisha Timu Hizi na KWA kuwahusisha wapenzi na mashabiki wake kupiga kura zitakazo wezesha Klabu hizi pendwa ziweze kujiendesha kibiashara.
Afisa mtendaji Mkuu Wa Klabu ya Simba Barbara Gonzalezi Amesifu Kampeni hii na Amesema Haya.. "Kwenye mambo ya kibiashara vilabu lazima tusimame pamoja."
Gonzalez meainisha kuwa fedha zote zitakazo patikana zitaelekezwa Katika Kuboresha miundo mbinu ya Klabu na hasa uwanja "Hela zote ambazo tutapata tutapeleka kwenye ujenzi wa uwanja"Aliongeza Barbara.
Naye Afisa habari wa Klabu Ya Simba Ahamed Ally Amesema Jambo la Leo nila tofauti kidogo kwani kampeni hii ina lengo la kuziletea maendeleo Klabu Zote mbili,Na amewahamasisha mashabiki na wapenzi wa Klabu ya Simba Kuendelea na zoezi la Uchangiaji kwani Wao walikwisha Anza hapo kabla kuchanga Ili kufanikisha ujenzi Wa miundo mbinu.
"Nani Zaidi ni kutunishiana misuli, nani anaweza kuchangia zaidi. Ameshasema CEO fedha tunapeleka kwenye miundombinu pale Bunju. Hatuwezi kufika huko kama mashabiki hawatajitokeza kuchangia kufanikisha hili la ujenzi." alimaliza Ahamed Ally
Kwa upande Wa Klabu ya Yanga Kupitia Kaimu Afisa mtendaji Mkuu Senzo Mazingisa Mbatha,Ameeleza Kuwa Kampeni hii imekuja Wakati muafaka na inaendana na agenda iliyopo ya kuifnya Klabu ya Yanga Kuwa Klabu ya kisasa na Yenye Weledi,Hivyo inapeswa kuchukuliaa mradi huu kwa Umakini na uzito wa kipekee, lakiniAmeongeza Kuwa,Hii haimaanishi Kuwa Shughuli zingine za Klabu zimeachwa bali Zote zinaendelea na hii Ni nyongeza ya Kati ya Shughuli nyingine zinazo endelea ndani ya Klabu Ili kuzidi kuijenga Klabu ya Yanga.
Senzo Anasema "Hatuwezi kuchukulia mradi huu kimzahamzaha sababu,Ni Mara ya kwanza inafanyika Hapa Tanzania,Pale Timu pinzani zinakutana kujadili masuala yatakayoziwezesha kupata Fedha"
"Si Suala la mashabiki kwenda viwanjani tu na kushangilia Timu Zao Lakini Klabu Hazinufaiki na chochote"
Amesisitiza Kuwa Ni Muda Wa Mashabiki wa Timu Zote Kupiga kura ilikuziwezesha Timu Zao kujimarisha kiuchumi.
Naye Afisa habari Yanga Haji Sundey Manara Ame wataka Mashabiki wa Yanga kupiga kura kwa Wingi Ili kuiwezesha Timu Yao kuzidi kuongoza Kama wanavyo Ongoza Kwenye Mashindano Mengine "Wanayanga Hatuna Jambo Dogo tupige kura tuweze kushinda Kama tulivyoshinda Mechi ya tarehe ishirini na nane pale Mwanza"Alisema Manara.
Kampeni hii ya Nani Zaid itaendeshwa Kupitia mitandao ya simu Ya Vodacom,Tigo na Airtel Tanzania Ambapo watumiaji wa Mitabdao Hiyo wataingia Katika mfumo wa kifedha wa mtandao husika Ili kuwezaa kushiriki.
Kuipigia Kura Klabu ya Simba kwa watumiaji wa Vodacom namba ya Kampuni ya Ni 002233 na Namba ya kumbukumbu ni 002233,Tigo Kumbukumbu Namba 776655 na KWA Airtel Namba ya Kampuni Namba 776655 na Kumbukumbu Namba 776655.
Kuipigia Kura Klabu ya Yanga kwa watumiaji wa Vodacom namba ya Kampuni Ni 004455 na Namba ya kumbukumbu ni 004455,Tigo Kumbukumbu Namba 887766 na KWA Airtel Namba ya Kampuni Namba 887766 na Kumbukumbu Namba 887766.
Comments
Post a Comment