Tangu Zama za kale Jamii Mbalimbali zilijiwekea utaratibu Wa kuhesabu Watu wake ili kubaini Idadi Yao na kuweza kuwapatia Mahitaji Yao ya Msingi na kugawanya Rasilimali za Jamii kwa Usawa.
Hata moja ya Vitabu vya iman imeeleza Namna Jamii ya Watu Wa walivyo weza kutekeleza zoezi la kuhesabiana ili kutambuana Kichwa kwa Kichwa Nyumba kwa Nyumba,ili Kuwa watambua Jamii ya ile Baada ya kutoka uhamishoni Misri. Uthibitisho wa Jambo Hili unaweza soma Katika Biblia Katika kitabu Cha Hesabu 1:2-3
Tanzania ikiwa Miongoni mwa Jamii iliyo Chini ya Dunia nayo imefuata utaratibu huu wa kuhesabiana Kama ilivyo fanyika hata Katika Jamii za kale Tangu Zama za Kale.
Sensa si zoezi geni hapa nchini Tanzania Kwani Miaka kadhaa iliyopita limefanyika, sensa ya kwanza ikiwa Ni Mwaka 1967, nakufuatiwa nazoezi la Sensa nyingine Kati ya mwaka 1978,1988, 2002 Na sensa ya Mwisho ilifanyika Agost, 2012.
Sensa itakayo fanyika Mapema Agosti 23,2022 itakua Ni sensa ya Sita Tangu Tanzania ipate uhuru wake Mwaka 1961,Ikiwa na lengo la kutambua idadi ya Watu nchini,Pamoja na kuisaidia Serikali kuandaa mipango yake na sera za Kimaendeleo ili kuweza kuwahudumia wananchi kikamilifu.
Serikali ya Tanzania Baada ya Kupata uhuru ilijiwekea utaratibu kisheria wa kuhesabiwa kila Baada ya Miaka 10,
Wakati Wa Zoezi Hili la Sensa,zipo Imani Mbali mbali Miongoni mwa baadhi ya Jamii,kwa kulihusisha Zoezi Hili na Imani potofu zinazojengeka Miongoni mwao.Zipo Jamii zilizojenga Imani Kuwa kuhesabiwa hupelekea Watu Kuja kushindwa kuzaliana,Na zipo Jamii huhusisha zoezi hili na Imani Kuwa kuhesabiwa Ni Dalili za Mwisho wa Dunia Au Kiama .Jamii zingine Zinaamini katika tamaduni zao Kuwa kuhesabiwa kwa Watu Ni kinyume na Imani za miungu wanayoiabudu na kuiamini,Na Jamii zingine zina husisha zoezi Hili la Sensa na ujio wa Dini Mpya ya Iluminati(Freemason)
Hakika Jamii Mbalimbali ndani ya Nchi zinapaswa kuelimishwa Juu ya umuhimu wa Zoezi Hili Adhimu la Sensa kwa kina kwa kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja, Familia,Ubalozi wa Nyumba kumikumi,Mtaa,kitongoji,Kijiji ngazi ya kata,Wilaya Mkoa Hadi Taifa Juu ya umuhimu na Faida ya Zoezi la Sensa.
Zoezi la Sensa au kwa Lugha Rahisi Kuhesabiana,Zoezi linalo tarajiwa Kufanyika Agosti 23,2022 linazo Faida Kubwa Katika Jamii na Taifa kwa ujumla.
Zoezi la Sensa litasaidia Kujua idadi ya Wananchi Nchi nzima, kwa Umri wao na Jinsia.
Zoezi la Sensa litasaidia Kutayarisha mipango ya maendeleo,Kupitia Takwimu zitakazo patikana zitatumika kuandaa Mipango na sera za Kimaendeleo,Zitakazo rahisisha kuainisha Misingi Katika kufanya Maamuzi Mbalimbali kwa idara za serikali na mashirika Binafsi Katika Maamuzi na uboreshaji wa huduma kulingana na idadi na mahitaji ya Makundi Mbali mbali yatakayo Kuwa yameainishwa na Takwimu za Sensa.
Sensa itasaidia kutoa picha halisi ya Hali ya Uchumi na kupima Hali ya Sasa ya Uchumi KWA ngazi ya mtu mmoja mmoja kaya,Mtaa,Kitongoji Kijiji kata na hata Wilaya kwa ujumla,kwa Kulinganisha Takwimu za Sasa na zile za miaka Iliyopita.
Sensa itasaidia Kuweka vipaumbele Katika Mgawanyo wa Rasilimali Katika maeneo Mbalimbali mathalani Kati ya maeneo ya mjini na vijijini kufuatana na Takwimu zitakazopatikana Katika zoezi la Sensa la Agosti 23 Mwaka huu.
Rai Yangu kwa Watanzania wenzangu,tuwape ushirikiano wataalamu watakaotutembelea Katika kaya zetu,Tujibu kwa usahihi Maswali yatakayo kuwa yameorodheshwa Katika Madodoso ya Sensa. Tusijiweke Mbali na zoez hili kwa iman Potofu zinazo jengwa na Baadhi ya Watu.
Hakika Yapo manufaa Mengi kupitia zoezi la Sensa,Wito na shime kwa Watanzania Wote kujiandaa kuhesabiwa,Sensa Ni maendeleo,Ewe Mtanzania jiandae kuhesabiwa ifikapo Agosti 23,2022
Comments
Post a Comment