Klabu ya Soka ya Simba katika Kampeni ya Nani zaidi ikihusisha watani Zao YANGA iliyozinduliwa mwanzoni mwa Mwezi huu, Inaendelea kujipatia kura na fedha mbele ya Watani Zao wa Jadi YANGA.
Hadi mapema leo Simba wanaongoza kwa Kura 30,102 dhidi ya Watani Zao YANGA wenye kura 24,795.Kwa matokeo hayo Simba Hadi Sasa Wamejikusanyia kiasi Cha Tsh.30,102,498 dhidi ya Watani zao YANGA waliojikusanyia jumla ya Tsh.24,795,395.
Je Hadi mwisho wa Kampeni hii Nani ataibuka mshindi? Endelea Kupigwa kura ili Uiwezeshe timu yako kushinda na Kuiwezesha timu yako kujiimarisha kiuchumi.
Comments
Post a Comment