Skip to main content

Posts

WANANCHI WAHIMIZWA KUZINGATIA USAFI WA MAZINGIRA.

  Mkuu wa Wilaya Kakonko kanali Evance Mesha Mallasa, amewataka Wananchi Wilayani Kakonko kujenga utamaduni wa kufanya usafi katika mazingira Ili kuufanya mji wa Kakonko Kuwa safi na wenye kuvutia. Ameyasema hayo Agosti 01 2023,katika  kikao Cha maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa uhuru kilicho fanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko. Kanali Mallasa  amewataka watumishi wa idara ya mazingira Kuwa Msatari wa Mbele kuwahamasisha wananchi kufanya usafi wa mazingira kama ambavyo viongozi wa Serikali wanasisitiza akiwamo Makamu Wa Rais Dkt Philip Isdory Mpango na vile vile kutekeleza Kwa vitendo ratiba ya kitaifa ya usafi ambapo Kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi inapaswa kutekelezwa. Aidha amekemea,Suala La baadhi ya Watumishi wa idara ya mazingira kushindwa Kutoa ushirikiano Kwa uongozi wa Wilaya hasa pale wanapo tafutwa kwaajiri ya kupatiwa Maelekezo ya utekelezaji wa Usafi wa Mazingira. "Viongozi kunabaadhi ya mambo tunapaswa kushirikishana,Sasa Unakuta umampi...
Recent posts

WANANCHI WAASWA KUFANYA MAZOEZI KUIMARISHA AFYA.

Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mesha Mallasa, amewaasa  wananchi Wilayani humo kujenga tabia ya kufanya Mazoezi na kushiriki Michezo mbalimbali Ili kuimarisha afya na kuepuka magonjwa mbali mbali. Kanali Mallasa ametoka wito huo,wakati wa kikao Cha sherehe za kukaribisha mbio za Mwenge kilichofanyika tarehe 18,Julai,2023 katika ukumbi wa Halmashauri Wilaya Kakonko. "Niwaombe Kila mkuu wa Idara  Taasisi hata Mwananchi mmojammoja  Kwa pamoja,kujitokeza kushiriki Mazoezi Ili kuimarisha afya na kuepukana na Magonjwa mbalimbali ambayo tiba yake inaweza Kuwa ni Mazoezi tu"ameeleza Kanali Mallasa Kwa upande mwingine Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko,Bw.Ndaki Stefano Mhuli,Amesema uongozi wa Halmashauri unatambua umuhimu wa Mazoezi na michezo kwa ujumla,hivyo umetenga siku ya Jumamosi kama siku maalum kwaajiri ya Watumishi wa Halmashauri kushiriki Mazoezi na Michezo,Ili kuimarisha afya zao. "Mhe.mkuu wa Wilaya niseme tu Jambo hili tunalichumilia kwa uzit...

ZIARA YAKUKAGUA MIRADI INAYOTARAJIWA KUZINDULIWA NA MBIOZA MWENGE MWAKA HUU

  Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mesha Mallasa,amewataka wataalam,wanaosimamia na kuratibu miradi mbali mbali ya maendeleo inayo tarajiwa Kuzinduliwa na Mbio za mwenge mapema mwezi Agosti Mwaka huu,kuhakikisha wanamaliza changamoto zilizobakia katika miradi hiyo ambayo itazimduliwa na mbio za Mwenge Wilayani Kakonko. Wito huo umetolewa  Julai 12,2023 wakati wa ziara ya kukagagua miradi hiyo inayoendelea  kutekelezwa. "Ndugu zangu,muda uliobaki wa kukamilisha na kuondoa dosari ndogo ndogo zilizopo ni Mchache kabla ya Ujio wa Mwenge wa Uhuru Wilayani kwetu,niwatake wataalamu wote wanaohusika na miradi hii,kujitahidi kuondoa changamoto tunazoziona,Ili kuepuka miradi kukataliwa na viongozi wa Mbio za Mwenge....itakua ni fedheha Kwa Wilaya na mkoa kwa ujumla kwani taswila halisi ya mkoa wa kigoma katika mbio za Mwenge mwaka huu itaonekana  Kuanzia Wilayani Kakonko"Alisema Kanali Mallasa. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko Bw.Ndaki Stefano Mhul...

KAMATI YA SIASA YA ZURU MIRADI WILAYANI KAKONKO.

Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa Kigoma,Ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mkoa Kigoma Bw.Malima Mobutu, imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani Kakonko,leo Juni 30,2023. Katika ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi, Mkuu wa Wilaya Kakonko  Kanali Evance Mesha Mallasa,ameambatana na Kamati ya Usalama Wilaya  Kakonko, Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya Kakonko pamoja na wakuu wa idara mbali mbali kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  Wilaya Kakonko. Akizungumza Wakati wa Majumuisho ya ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Mkoa Kigoma Bw.Mobutu ameeleza namna Kamati ya siasa ilivyoridhishwa na namna miradi hiyo inavyoendelea kutekelezwa Wilayani Kakonko,na amewataka watendaji kurekebisha kasoro ndogo ndogo zilizo bainika katika Miradi iliyotembelewa na miradi mingine Yote inayoendelea kutekelezwa. "Kwa niaba ya Kamati ya siasa ya Chama,nitumie Fursa hii kuwapongeza watendaji wote,na kwa ujumla nis...

WANANCHI WILAYANI KAKONKO WAHIMIZWA KUTUNZA MIUNDOMBINU.

Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mesha Mallasa, Leo Juni,28,2023,amewaasa Wananchi  wilayani kakonko kuitunza miundombinu mbalimbali ilinayowekwa na serikali Ili kuwahudumia Wananchi.  Kanali Mallasa Ametoa wito Huo wakati akipokea daraja la Muda la Chuma lililojengwa katika mto Muhwazi Barabara ya Kakonko - Ikambi linalounganisha Shule ya Sekondari Ikambi na kata ya Kakonko mjini,ambalo Ujenzi wake umetekelezwa na kamandi ya Magharibi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kushirikiana na TARURA Wilaya Kakonko. Akizungumza wakati wa kupokea daraja hilo Kanali Mallasa,Amelishukuru Jeshi la Wananchi wa Tanzania pamoja na TARURA kwa ujenzi wa daraja hilo ambalo ni kiungo muhimu kwa huduma za Jamii ikiwemo Shule ya Sekondari Ikambi. Aidha Amewasisitiza Wananchi  Wilayani Kakonko hususani wa Kijiji Cha Itumbiko na kata nzima ya Kakonko kuitunza miundombinu ya daraja hillo Ili  iweze kudumu na kuwahudumia  Wananchi kwa ufanisi. "Niwaombe Wananchi Pamoja na TARURA, ...

MKUU WA WILAYA YA KAKONKO AKAGUA MIRADI 07 ITAKAYOTEMBELEWA NA MWENGE WA UHURU 2023.

  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Evance Mallasa kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wa Wilaya amekagua miradi 07 itakayotembelewa na mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2023 na kusisitiza mapungufu yaliyoonekana katika miradi hiyo kufanyiwa kazi. Col.Mallasa amefanya ziara hiyo siku ya jumatano Mei 31, 2023 akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama, Viongozi wa chama cha mapinduzi CCM (W), Katibu wa Mbunge, Wakuu wa Taasisi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri. Katika ziara hiyo viongozi walitembelea Shule ya Sekondari ya Wasichana Kakonko, Ujenzi wa  Wodi tatu za Hospitali ya Wilaya Kakonko, Kiwanda Cha Uzalishaji Mkaa mbadala,Ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya (IKulu ndogo), Ujenzi wa Ofisi ya Afisa Tarafa Kasanda, Kikundi Cha wanunuzi wa mazao ya nafaka Kiziguzigu  Pamoja na Kituo Cha Mafuta Glory to God. Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2023 unatarajiwa kukimbizwa Wilayani Kakonko tarehe 16 Agosti, 2023 na kupokelewa Kimkoa Wilayani Kakonko uk...

MAANDALIZI YA MBIO ZA MWENGE YAANZA WILAYANI KAKONKO

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Aggrey Magwaza amefanya kikao cha kwanza cha Kamati ya maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 na kupitisha miradi itakayopitiwa na kutembelewa na Mwenge wa Uhuru utakaokimbizwa Wilayani Kakonko tarehe 16 Agosti, 2023. Col. Aggrey Magwaza ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo anayekaimu nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Kakonko amekutana na wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko leo Mei 17, 2023. Miradi iliyopendekezwa na kupitishwa kutembelewa na Mwenge wa Uhuru 2023   ni  Uzinduzi wa vyumba 08 vya madarasa na ofisi 3 za waalimu shule ya Sekondari ya wasichana Kakonko, Kutembelea kikundi cha Vijana bodaboda Muganza, Uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza mkaa mbadala kikundi cha Vijana Itumbiko, Kuweka jiwe la Msingi nyumba ya Mkuu wa Wilaya (Ikulu ndogo Kakonko) inayojengwa Itumbiko, Kukagua Barabara ya lami Kakonko-Itumbiko inayoelekea hospitali ...