Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col.Evance Mallasa kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wa Wilaya amekagua miradi 07 itakayotembelewa na mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2023 na kusisitiza mapungufu yaliyoonekana katika miradi hiyo kufanyiwa kazi.
Col.Mallasa amefanya ziara hiyo siku ya jumatano Mei 31, 2023 akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama, Viongozi wa chama cha mapinduzi CCM (W), Katibu wa Mbunge, Wakuu wa Taasisi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri.
Katika ziara hiyo viongozi walitembelea Shule ya Sekondari ya Wasichana Kakonko, Ujenzi wa Wodi tatu za Hospitali ya Wilaya Kakonko, Kiwanda Cha Uzalishaji Mkaa mbadala,Ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya (IKulu ndogo), Ujenzi wa Ofisi ya Afisa Tarafa Kasanda, Kikundi Cha wanunuzi wa mazao ya nafaka Kiziguzigu Pamoja na Kituo Cha Mafuta Glory to God.
Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2023 unatarajiwa kukimbizwa Wilayani Kakonko tarehe 16 Agosti, 2023 na kupokelewa Kimkoa Wilayani Kakonko ukitokea Mkoani Kagera.
Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 ni "Tunza Mazingira, okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa Taifa".
Comments
Post a Comment