Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mesha Mallasa,amewataka wataalam,wanaosimamia na kuratibu miradi mbali mbali ya maendeleo inayo tarajiwa Kuzinduliwa na Mbio za mwenge mapema mwezi Agosti Mwaka huu,kuhakikisha wanamaliza changamoto zilizobakia katika miradi hiyo ambayo itazimduliwa na mbio za Mwenge Wilayani Kakonko.
Wito huo umetolewa Julai 12,2023 wakati wa ziara ya kukagagua miradi hiyo inayoendelea kutekelezwa.
"Ndugu zangu,muda uliobaki wa kukamilisha na kuondoa dosari ndogo ndogo zilizopo ni Mchache kabla ya Ujio wa Mwenge wa Uhuru Wilayani kwetu,niwatake wataalamu wote wanaohusika na miradi hii,kujitahidi kuondoa changamoto tunazoziona,Ili kuepuka miradi kukataliwa na viongozi wa Mbio za Mwenge....itakua ni fedheha Kwa Wilaya na mkoa kwa ujumla kwani taswila halisi ya mkoa wa kigoma katika mbio za Mwenge mwaka huu itaonekana Kuanzia Wilayani Kakonko"Alisema Kanali Mallasa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko Bw.Ndaki Stefano Mhuli,amewaelekeza wataalam mbalimbali katika miradi hiyo kuweka kambi katika miradi hiyo Ili kushughulikia changamoto hizo,pamoja na kutoa taarifa ya Kila kinacho endelea kwa muda wote wanapokua katika maeneo ya miradi.
Miradi hiyo ni Ujenzi wa vymba 8 vya madarasa na ofisi 3 za walimu Shule ya wasichana Kakonko,Kiwanda Cha kutengeneza mkaa mbadala Itumbiko,ujenzi wa Ikulu ndogo Kakonko,Barabara ya Lami Kakonko -Itumbiko,Kituo Cha Mafuta Glory to God,Klabu ya wapinga Rushwa Shule ya Sekondari Buyungu,Ujenzi wa Ofisi ya Afisa Tarafa Kasanda, na Zahanati ya Ilabiro kata ya Gwanumpu
Comments
Post a Comment