Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa Kigoma,Ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mkoa Kigoma Bw.Malima Mobutu, imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani Kakonko,leo Juni 30,2023.
Katika ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi, Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mesha Mallasa,ameambatana na Kamati ya Usalama Wilaya Kakonko, Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya Kakonko pamoja na wakuu wa idara mbali mbali kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya Kakonko.
Akizungumza Wakati wa Majumuisho ya ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Mkoa Kigoma Bw.Mobutu ameeleza namna Kamati ya siasa ilivyoridhishwa na namna miradi hiyo inavyoendelea kutekelezwa Wilayani Kakonko,na amewataka watendaji kurekebisha kasoro ndogo ndogo zilizo bainika katika Miradi iliyotembelewa na miradi mingine Yote inayoendelea kutekelezwa.
"Kwa niaba ya Kamati ya siasa ya Chama,nitumie Fursa hii kuwapongeza watendaji wote,na kwa ujumla niseme tu,tumeridhishwa na namna miradi tuliyo tembelea inavyo endelea kutekelezwa Wilayani Kakonko" Alisema Bw.Mobutu
Aidha Amewataka wananchi Wote Wilayani Kakonko kudumisha Amani na Usalama Ili kuchochea zaidi Maendeleo.
Naye Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Mallasa, Amewataka watumishi na watendaji wote Wilayani kakonko kufanya kazi kwa weledi Ili kuifikia adhima njema ya Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko Bw.Ndaki Stefano Mhuli,ameeleza kuwa amewachukulia hatua za kinidhamu na Wengine za kisheria Ikiwamo kuwafukiza kazi watendaji waliobainika kuhusika na upotevu vifaa vya miradi ya maendeleo.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Bweni la Wanafunzi 120,Shule ya wasichana Kakonko Sekondari, Ujenzi wa Wodi tatu za wagonjwa Hospitali ya Wilaya Kakonko,Daraja la Chuma la Muda katika Mto Muhwazi Itumbiko, Ujenzi wa Barabara ya lami Kakonko -Itumbiko (Km 1.2),Ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya (Ikulu Ndogo),Chanzo Cha Maji Nyakayenzi pamoja na Mradi wa Stendi ya Mabasi Wilaya Kakonko, Mradi ambao umesimama kwa muda mrefu.
Comments
Post a Comment