Mkuu wa Wilaya Kakonko kanali Evance Mesha Mallasa, amewataka Wananchi Wilayani Kakonko kujenga utamaduni wa kufanya usafi katika mazingira Ili kuufanya mji wa Kakonko Kuwa safi na wenye kuvutia.
Ameyasema hayo Agosti 01 2023,katika kikao Cha maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa uhuru kilicho fanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko.
Kanali Mallasa amewataka watumishi wa idara ya mazingira Kuwa Msatari wa Mbele kuwahamasisha wananchi kufanya usafi wa mazingira kama ambavyo viongozi wa Serikali wanasisitiza akiwamo Makamu Wa Rais Dkt Philip Isdory Mpango na vile vile kutekeleza Kwa vitendo ratiba ya kitaifa ya usafi ambapo Kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi inapaswa kutekelezwa.
Aidha amekemea,Suala La baadhi ya Watumishi wa idara ya mazingira kushindwa Kutoa ushirikiano Kwa uongozi wa Wilaya hasa pale wanapo tafutwa kwaajiri ya kupatiwa Maelekezo ya utekelezaji wa Usafi wa Mazingira.
"Viongozi kunabaadhi ya mambo tunapaswa kushirikishana,Sasa Unakuta umampigia simu Mtu wa Idara ya mazingira umshirikishe jambo la usafi wa mazingira yetu hapokei simu Wala hakutafuti hata Baada ya kuona simu Yako Wala Ujumbe mfupi hajibu pale Unapo mtumia..,niwaombe tubadilike"Alisema Kanali Mallasa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko Ndaki Stephano Mhuli ameahidi Kufuatilia kwa karibu na kutekeleza maagizo yaliyotolewa kupitia idara ya mazingira Ili kuhakikisha mji wa Kakonko unakuwa Safi na wenye kuvutia muda Wote.
Comments
Post a Comment