Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mesha Mallasa, Leo Juni,28,2023,amewaasa Wananchi wilayani kakonko kuitunza miundombinu mbalimbali ilinayowekwa na serikali Ili kuwahudumia Wananchi.
Kanali Mallasa Ametoa wito Huo wakati akipokea daraja la Muda la Chuma lililojengwa katika mto Muhwazi Barabara ya Kakonko - Ikambi linalounganisha Shule ya Sekondari Ikambi na kata ya Kakonko mjini,ambalo Ujenzi wake umetekelezwa na kamandi ya Magharibi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kushirikiana na TARURA Wilaya Kakonko.
Akizungumza wakati wa kupokea daraja hilo Kanali Mallasa,Amelishukuru Jeshi la Wananchi wa Tanzania pamoja na TARURA kwa ujenzi wa daraja hilo ambalo ni kiungo muhimu kwa huduma za Jamii ikiwemo Shule ya Sekondari Ikambi.
Aidha Amewasisitiza Wananchi Wilayani Kakonko hususani wa Kijiji Cha Itumbiko na kata nzima ya Kakonko kuitunza miundombinu ya daraja hillo Ili iweze kudumu na kuwahudumia Wananchi kwa ufanisi.
"Niwaombe Wananchi Pamoja na TARURA, na viongozi Wote wa kata tushirikiane kwa pamoja kulitunza daraja hili,na miundombinu hii tuitunze Ili itutunze" Alisema Kanali Mallasa.
"Hivi vyuma vilivyo jenga daraja hili ni Mali ya Jeshi,Kama ni Mali ya Jeshi Maana yake ni Mali ya serikali,uharibifu wa vyuma hivi Kwa Namna yeyote Ile itakuwa ni kuihujumu serikali inayojitahidi kuwahudumia Wananchi wake" Aliongeza Kanali Mallasa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko Ndaki S.Mhuli,Ameahidi kushirikiana na Wananchi wa eneo la Itumbiko na kata ya Kakonko Kuilinda miundombinu ya daraja Ili liweze kutoa huduma Kwa Wananchi.
"Mhe.Mkuu wa Wilaya,tukuahidi,tutashirikiana na wananchi ilikulinda miundombinu ya daraja hili ambalo limejengwa na vijana wetu wazalendo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania,Wengine tumebaki na mshangao kwani tuliamini vyuma hivi vingehitaji mashine za kuvibeba Ili viwezekufungwa lakini ni Vijana wetu hawa wazalendo kwa uchache wao wamevifunga na daraja limekamilika "aliongeza Mkurugenzi Ndaki
Daraja lililojengwa na kukabidhiwa Kwa Mkuu wa Wilaya linauwezowa kupitisha magari ya tani arobaini bila changamoto yoyote.
Daraja la Mto Muhwazi lilisombwa na maji Aprili 10,2023 kufuatia Mvua kubwa zilizonyesha na kupelekea wanafunzi miambili (200) wa Shule ya Ikambi kushindwa kuhudhuria masomo, pamoja na Wananchi kushindwa kuvusha mazao yao toka Mashambani.
Comments
Post a Comment