Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mesha Mallasa, amewaasa wananchi Wilayani humo kujenga tabia ya kufanya Mazoezi na kushiriki Michezo mbalimbali Ili kuimarisha afya na kuepuka magonjwa mbali mbali.
Kanali Mallasa ametoka wito huo,wakati wa kikao Cha sherehe za kukaribisha mbio za Mwenge kilichofanyika tarehe 18,Julai,2023 katika ukumbi wa Halmashauri Wilaya Kakonko.
"Niwaombe Kila mkuu wa Idara Taasisi hata Mwananchi mmojammoja Kwa pamoja,kujitokeza kushiriki Mazoezi Ili kuimarisha afya na kuepukana na Magonjwa mbalimbali ambayo tiba yake inaweza Kuwa ni Mazoezi tu"ameeleza Kanali Mallasa
Kwa upande mwingine Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko,Bw.Ndaki Stefano Mhuli,Amesema uongozi wa Halmashauri unatambua umuhimu wa Mazoezi na michezo kwa ujumla,hivyo umetenga siku ya Jumamosi kama siku maalum kwaajiri ya Watumishi wa Halmashauri kushiriki Mazoezi na Michezo,Ili kuimarisha afya zao.
"Mhe.mkuu wa Wilaya niseme tu Jambo hili tunalichumilia kwa uzito,Ili kuimarisha Afya, ...Mazoezi ni lazima kwa kila mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko,Michezo ni Afya na ni undugu pia" amesema Bwa.Ndaki.
Mwenge wa Uhuru unatarajia kuingia Mkoani Kigoma Tarehe 16,Agosti 2023, ambapo utapokelewa Wilayani Kakonko na kizindua miradi Mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo.
Comments
Post a Comment