Serikali ya Jamuhuhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imepokea mkopo wa Dola za Marekani Milioni 775 (tsh trilion 1.8) Kutoka Benki ya Dunia. Taarifa Rasimi Kutoka Wizara ya Fedha na Mipango,inasema Fedha hizo za mkopo na msaada wa masharti nafuu zimetolewa Kwa Serikali ya Tanzania kwaajiri ya kusaidia Utekelezaji wa Bajeti,Kuboresha Uchumi na Huduma za afya. Aidha Wizara imeainisha mchanganuo wa Fedha hizo Kuwa Dola za marekani milioni 500 (Sawa na shilingi trilioni 1.1)zitatolewa na shirika la kimataifa la Maendeleo(IDA), kwa ajiri ya kufufua uchumi ulio athiriwa na mlipuko wa Ugonjwa wa UVIKO 19 pamoja na Vita vinavyo endelea kati ya Urusi na Ukiraine. Vile vile Dola za Marekani milioni 25 (sh.bilioni 58.1) zitatolewa kama Msaada na mfuko Wa Dunia wa kusaidia Wanawake,Vijana na watoto. Wizara imeainisha Matumizi ya Fedha zote kuwa,Dola milioni 250(sh.Bilioni 581) Zitatumika kwaajiri ya Program ya Afya ya mama na mtoto Kwa njia ya kupima ...