Jumla ya wanafunzi 264 kutoka shule tano za Mkoa wa Kagera ambazo zilifutiwa matokeo na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), wanatarajiwa kurudia mtihani wa kuhitimu darasa la saba kuanzia Disemba 21 hadi 22 mwaka huu.
Wanafunzi hao watakaorudia mtihani huo ni kutoka katika shule za msingi Jamia, Rweikiza na Karume zilizopo Wilaya ya Bukoba, Kazoba iliyopo Wilaya ya Karagwe na St. Severin iliyopo wilaya ya Biharamulo.
Afisa Elimu Mkoa wa Kagera, Kharifa Shemahonge amesema kuwa maandalizi ya kurudia mtihani huo yamekamilika.
Source: UFM RADIO#UFMUpdates
Comments
Post a Comment