Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limethibitisha kuwafikisha mahakamani watu 11 kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa dawa na vifaa tiba katika maeneo ya kutolea huduma za afya na kupelekea wananchi kukosa dawa kwa wakati
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP Filimon Makungu amethibitisha kufikishwa mahakamani kwa watu hao katika mkutano wa kwanza wa kamati ya ushauri ya mkoa kwa mwaka 2022 - 2023 na kuwataka watumishi wa umma kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa sheria
Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma Daktari Jesca Lebba amesema wizi wa dawa na vifaa tiba unarudisha nyuma utendaji kazi kwa wananchi na kwamba katika maeneo ambayo wizi umefanyika huduma zimekuwa za kusuasua.
Aidha Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ameagiza kuendelea kufanyika uchunguzi wa kina na kubaini dawa zote zinazoingia kama zinatumika kwa ukamilifu kwa lengo la kukomesha wizi huo
SOURCE: #EastAfricaRadio
Comments
Post a Comment