Rais wa Afrika Kusini Cylil Ramaphosa amechaguliwa Kwa mara nyingine kukiongoza Chama tawala Cha Afrika Kusini African National Congress (ANC).
Katika uchaguzi huo,Rais Ramaphosa Amembwaga mpinzani wake wa karibu Bw.Zweli Mkhize Kwa Kura 2,476 Dhidi ya Kura 1,897.
Ramaphosa Ameshinda kinya'ganyiro hicho licha ya Shutuma za Ufisadi na matumizi mabaya ya Fedha,zilizomkabiri wiki kadhaa zilizopita na kuamsha taharuki ndani ya Bunge la Afrika Kusini.
Ramaphosa Sasa anajiweka katika nafasi nzuri ya kukiongoza Chama Cha ANC katika uchaguzi ujao wa Mwaka 2024,Licha ya kuwa vyombo vya usalama na ofisi ya Ushuru na Benki kumchunguza juu ya madai ya kuficha kiasi kikubwa Cha fedha katika Shamba lake.
Comments
Post a Comment