Serikali ya Jamuhuhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imepokea mkopo wa Dola za Marekani Milioni 775 (tsh trilion 1.8) Kutoka Benki ya Dunia.
Taarifa Rasimi Kutoka Wizara ya Fedha na Mipango,inasema Fedha hizo za mkopo na msaada wa masharti nafuu zimetolewa Kwa Serikali ya Tanzania kwaajiri ya kusaidia Utekelezaji wa Bajeti,Kuboresha Uchumi na Huduma za afya.
Aidha Wizara imeainisha mchanganuo wa Fedha hizo Kuwa Dola za marekani milioni 500 (Sawa na shilingi trilioni 1.1)zitatolewa na shirika la kimataifa la Maendeleo(IDA), kwa ajiri ya kufufua uchumi ulio athiriwa na mlipuko wa Ugonjwa wa UVIKO 19 pamoja na Vita vinavyo endelea kati ya Urusi na Ukiraine.
Vile vile Dola za Marekani milioni 25 (sh.bilioni 58.1) zitatolewa kama Msaada na mfuko Wa Dunia wa kusaidia Wanawake,Vijana na watoto.
Wizara imeainisha Matumizi ya Fedha zote kuwa,Dola milioni 250(sh.Bilioni 581) Zitatumika kwaajiri ya Program ya Afya ya mama na mtoto Kwa njia ya kupima matokeo (PfoR) inayotekelezwa Tanzania Bara,na Dola za Marekani milioni 25(sh.Bilioni 58.1) Zitatumika kwaajiri ya mradi wa Uwekezaji kiuchumi(IPF) Kwa upande wa Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba Amesema kuwa Fedha hizo zinatarajiwa kuanza kuingia nchini mapema Mwishoni mwa juma hili (Ijumaa).
Benki ya Dunia imetoa Fedha za msaada wa kibajeti ikiwa ni baada ya kipindi Cha miaka 8 iliyopita tangu Tanzania inufaike na Msaada huo.
Aidha Benki ya Dunia Pamoja na Shirika la Fedha duniani (IMF) limeipongeza Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Raisi Dkt.Samia Suluhu Hasan Kwa usimamizi wa Uchumi wake kwa uwazi na uwajibikaji Ambao umezidi kuimarika, licha ya kuwepo athari za UVIKO 19 na Vita vya Urusi na Ukiraine.
Vilevile Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani limezisifu Sera za kiuchumi na kifedha za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Chini ya awamu ya sita ya Raisi Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Comments
Post a Comment