Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda, ameukataa mradi wa bwawa la maji katika Kijiji cha Zebeya Wilaya ya Maswa humo lililofanyiwa ukarabati kwa gharama ya Sh Milioni 754 akitilia shaka matumizi ya fedha hizo ikilinganishwa na kazi iliyofanyika
RC Nawanda, amefika na kujionea ukarabati wa Bwawa hilo na kudai fedha zilizotumika hazilingani na kazi iliyofanyika
"Mimi nimekuja kuona huu mradi wenu. Mimi nimekuja hapa bila kumuonea mtu. Mimi mwenzenu naungana na wananchi wenzangu mimi sijaridhishwa na huu mradi hata kidogo kwa hizo fedha Milioni 754, zilizotumika hapa (kukarabati) mimi sijaridhika nazo," amesema RC Nawanda
Mapema wakizungumzia ukarabati wa Bwawa hilo, mmoja wa wa wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Zebeya, diwani pamoja na Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Stanslaus Nyongo, wamesema mradi huo unastahili kuhojiwa juu ya matumizi ya Sh Milioni 754, hali iliyoungwa mkono na mkuu wa mkoa huo
Comments
Post a Comment