Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hasani,Amefanya uteuzi wa makatibu wakuu wa Wizara mbili,Ambazo ni Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara pamoja Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi,Leo Desemba 14,2022
Raisi Samia Amemteua Dkt. Hashil Twaib Abdalah Kuwa katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara, Pamoja na Bw. Kaspar Kaspar Mmuya Kuwa katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi.
Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Abdalah alikua Naibu katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara.
Naye Bw.Mmuya kabla ya Uteuzi huo alikua Naibu katibu Mkuu,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu)
Bwana Kaspar Kaspar Mmuya anakwenda kuziba nafasi ya Mbarak Abdulwakil aliuekuwa katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kufuatia kifo chake kilichotokea Novemba 30,2022 Zanzibar.
Aidha taarifa iliyo tolewa na Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu,Imeeleza Uteuzi huo unaanzia tarehe 9 Desemba,2022.
Comments
Post a Comment