Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2023

IMANI KAJULA MTENDAJI MPYA SIMBA

Klabu ya Simba  imemtambulisha Imani Kajula kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa klabu hiyo kwa mkataba wa miezi sita, akichukua nafasi ya Barbara Gonzalez aliyejiondoa. Kajula ni mzoefu kwenye uongozi wa mpira kwani alikuwepo kwenye Kamati ya maandalizi ya Michuano ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 17 yaliyofanyika nchini mwaka 2019. Kwa mujibu wa Meneja wa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema mkataba huo unaweza kurefushwa endapo Bodi itaridhishwa na utendaji wake katika kipindi cha miezi sita waliyompatia hivi sasa. Kajula alikuwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Masoko na Mawasiliano ya EAG Group tangu mwaka 2013. Pia amewahi kuwa Meneja Masoko wa Benki ya CRDB, Mkurugenzi wa Masoko na Biashara Benki ya Posta, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano Benki ya NMB. Chanzo: HABARI LEO

MAAFISA WA POLISI AMBAO HAWAJAOLEWA RUKSA KUBEBA MIMBA

Mahakama nchini Nigeria imeifuta sheria ya polisi iliyokuwa inakataza maafisa wake wa kike wasioolewa kubeba mimba Sheria hiyo awali ilikuwa inataka kuachishwa kazi kwa afisa yoyote ambaye amepata ujauzito na bado hajaolewa lakini Jaji wa mahakama hiyo amesema sheria hiyo ni ya kibaguzi kinyume cha sheria, batili na haifai Hukumu hiyo imetokana na shtaka la polisi mwanamke aliyefukuzwa kazi ambaye alipinga kuachishwa kazi kwake kwa misingi ya ubaguzi kwa vile wenzake wa kiume hawajafukuzwa kazi katika mazingira kama hayo  Chanzo :# EastAfricaRad io

GAVANA BENKI KUU ASTAAFU UTUMISHI

Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga Amemaliza kipindi chake Cha Utumishi Kwa Mujibu wa Sheria za Utumishi wa Nchi. Kufuatia Pro.Luoga Kumaliza kipindi chake Cha utumishi, Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hasani Amemteua Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba,Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Kuwa Gavana wa Benki kuu ya Tanzania (BoT). Vile vile Rais Dkt.Samia,Amemteua Dkt.Natu El- Maamry Mwamba,Kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.Kabla ya Uteuzi huo Dkt.Mwamba alikua Mhadhiri Mwandamizi wa chuo kikuu Cha Dar-es-Salaam na mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya uendeshaji wa Kiwanja Cha ndege Cha Kilimanjaro (KADCO). Dkt.Mwamba Anachukua Nafasi ya Bw.Emmanuel Mpawe Tutuba,Aliyeteuliwa Kuwa Gavana wa Benki kuu Ya Tanzania. Source:  Ikulu.go.tz . 

UTEUZI WA DIWANI WATENGULIWA

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan  Ametengua Uteuzi wa Kamishina Diwani Athuman Msuya,aliyemteua kuwa Katibu Mkuu Ikulu,tangu Januari 3,2023. Mhe.Rais Samia Ametengua Uteuzi huo mapema Leo Januari 5,2023,na badala yake Amemteua Bw.Mululi Majula Mahendeka Kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Kabla ya Uteuzi huu Bw.Majula alikua Afisa muandamizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu. Picha Kwa Hisani ya  Ikulu.go.tz

TISS YAPATA BOSS MPYA.

  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, Amemteua Bw.Said Hussein Masoro kuwa Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa taifa,Kuchukua nafasi ya Kamishina Diwani Athuman Msuya  Ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Kabla ya Uteuzi huo Bw.Masoro alikua akihudumu katika Idara ya Usalama wa Taifa kama Naibu Mkurugenzi mkuu na Mkurugenzi wa shughuli za  ndani wa Usalama wa Taifa. Wakati huo huo Rais Dkt.Samia amemteua Balozi Hussein Othman Katanga Kuwa Balozi wa Tanzania mjini New York, Nchini Marekani na muwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa. Balozi Katanga anachukia nafasi ya Balozi Profesa Kennedy Gaston,Ambaye Uteuzi wake umetenguliwa. Balozi Katanga kabla ya Uteuzi huu alikua Katibu Mkuu Kiongozi. Vile vile Mhe.Rais Dkt.Samia amemteua Bw.Moses Mpogole Kusiluka Kuwa Katibu Mkuu Kiongozi,Ambapo kabla ya Uteuzi huo alikua Katibu Mkuu Ikulu. Taarifa Rasimi Kutoka Kurugenzi ya mawasiliano ya Raisi Ikulu iliyotolewa mapema Jana Januari 3,2023, i...

SIMBA YASHUSHA MBRAZILI

    Klabu ya soka ya Simba,Imemtamgaza Oswaldo Roberto Oliveira "Robertinho" (70) kuwa kocha Mkuu wa klabu hiyo yenye makazi yake mitaa ya msimbazi Kariakoo Jijini Dar-es-Salaam. Robertinho,Anakuja Kuwa Mwalimu Mkuu wa Klabu ya Simba,kujaza  nafasi  Juma Ramadhan Mugunda Ambaye alikua akikaimu nafasi hiyo Kwa Muda. Kabla ya kujiunga na Klabu ya Simba Oliveira alikua akiinoa Klabu ya  Vipers ya nchini Uganda na Kuiwezesha  kutwaa Mataji mawili nchini Uganda katika msimu Uliopita,Vilevile ameisaidia Vipers kutinga hatua ya makundi Klabu Bingwa Afrika kwa mara ya Kwanza kwa kuiondosha Klabu ya Tp Mazembe ya nchini DR Congo. Klabu ya Simba imeingia Kandarasi ya miaka miwili na Mwalimu Oliveira  kuinoa miamba hiyo ya soka nchini Tanzania. Aidha,Oliveira Amekua na Rekodi ya kuvutia ndani ya Vipers Katika msimu Uliopita Ameiongoza Vipers kwa Jumla ya Michezo 57 Ameshinda Michezo 43 sare 9,Kupoteza 6 Magoli ya kufunga 99 na Ameiwezesha kutwaa vikombe 2 nchini ...