Klabu ya soka ya Simba,Imemtamgaza Oswaldo Roberto Oliveira "Robertinho" (70) kuwa kocha Mkuu wa klabu hiyo yenye makazi yake mitaa ya msimbazi Kariakoo Jijini Dar-es-Salaam.
Robertinho,Anakuja Kuwa Mwalimu Mkuu wa Klabu ya Simba,kujaza nafasi Juma Ramadhan Mugunda Ambaye alikua akikaimu nafasi hiyo Kwa Muda.
Kabla ya kujiunga na Klabu ya Simba Oliveira alikua akiinoa Klabu ya Vipers ya nchini Uganda na Kuiwezesha kutwaa Mataji mawili nchini Uganda katika msimu Uliopita,Vilevile ameisaidia Vipers kutinga hatua ya makundi Klabu Bingwa Afrika kwa mara ya Kwanza kwa kuiondosha Klabu ya Tp Mazembe ya nchini DR Congo.
Klabu ya Simba imeingia Kandarasi ya miaka miwili na Mwalimu Oliveira kuinoa miamba hiyo ya soka nchini Tanzania.
Aidha,Oliveira Amekua na Rekodi ya kuvutia ndani ya Vipers Katika msimu Uliopita Ameiongoza Vipers kwa Jumla ya Michezo 57 Ameshinda Michezo 43 sare 9,Kupoteza 6 Magoli ya kufunga 99 na Ameiwezesha kutwaa vikombe 2 nchini Uganda.
Comments
Post a Comment