Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga Amemaliza kipindi chake Cha Utumishi Kwa Mujibu wa Sheria za Utumishi wa Nchi.
Kufuatia Pro.Luoga Kumaliza kipindi chake Cha utumishi, Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hasani Amemteua Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba,Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Kuwa Gavana wa Benki kuu ya Tanzania (BoT).
Vile vile Rais Dkt.Samia,Amemteua Dkt.Natu El- Maamry Mwamba,Kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.Kabla ya Uteuzi huo Dkt.Mwamba alikua Mhadhiri Mwandamizi wa chuo kikuu Cha Dar-es-Salaam na mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya uendeshaji wa Kiwanja Cha ndege Cha Kilimanjaro (KADCO).
Dkt.Mwamba Anachukua Nafasi ya Bw.Emmanuel Mpawe Tutuba,Aliyeteuliwa Kuwa Gavana wa Benki kuu Ya Tanzania.
Source: Ikulu.go.tz
.
Comments
Post a Comment