Klabu ya Simba imemtambulisha Imani Kajula kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa klabu hiyo kwa mkataba wa miezi sita, akichukua nafasi ya Barbara Gonzalez aliyejiondoa.
Kajula ni mzoefu kwenye uongozi wa mpira kwani alikuwepo kwenye Kamati ya maandalizi ya Michuano ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 17 yaliyofanyika nchini mwaka 2019.
Kwa mujibu wa Meneja wa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema mkataba huo unaweza kurefushwa endapo Bodi itaridhishwa na utendaji wake katika kipindi cha miezi sita waliyompatia hivi sasa.
Kajula alikuwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Masoko na Mawasiliano ya EAG Group tangu mwaka 2013. Pia amewahi kuwa Meneja Masoko wa Benki ya CRDB, Mkurugenzi wa Masoko na Biashara Benki ya Posta, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano Benki ya NMB.
Chanzo: HABARI LEO
Comments
Post a Comment