Mahakama nchini Nigeria imeifuta sheria ya polisi iliyokuwa inakataza maafisa wake wa kike wasioolewa kubeba mimba
Sheria hiyo awali ilikuwa inataka kuachishwa kazi kwa afisa yoyote ambaye amepata ujauzito na bado hajaolewa lakini Jaji wa mahakama hiyo amesema sheria hiyo ni ya kibaguzi kinyume cha sheria, batili na haifai
Hukumu hiyo imetokana na shtaka la polisi mwanamke aliyefukuzwa kazi ambaye alipinga kuachishwa kazi kwake kwa misingi ya ubaguzi kwa vile wenzake wa kiume hawajafukuzwa kazi katika mazingira kama hayo
Chanzo :#EastAfricaRadio
Comments
Post a Comment