MAHAKAMA ya Mkoa wa Mbeya imemhukumu kifungo cha Miaka 30 jela Mkazi wa Isanga Jijini Mbeya, Hamad Yusufu, kwa kosa la Kuzini na Binti yake na Kuzaa naye mtoto mmoja wa Kike. Baba huyo anadaiwa kuanza kuzini na binti yake mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka 11 akimtisha kwa kutumia panga na kumpa ujauzito miaka mitano baadaye na kusababisha akatishe masomo ya elimu ya msingi. Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Gilbert Ndeuruo, amesema Mahakama imezingatia zaidi ushahidi uliotolewa na mtoto wa mshitakiwa huyo, Hadija Yusufu, anayedaiwa kuzini na kuzaa naye mtoto mmoja, Eva Yusufu, aliyethibitisha bila shaka kuwa baba yake alimlazimisha kuzini naye akimtishia kwa panga kwa zaidi ya miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2012, alipopata ujauzito. Pia Hakimu Ndeuruo, amesema mahakama hiyo imeridhika bila shaka kuwa mshtakiwa Hamad amefanya kosa hilo baada ya vipimo vya vinasaba yaani DNA vilivyowasilishwa Mahakamani hapo na Afisa kutoka Ofisi ya...