MAHAKAMA
ya Mkoa wa Mbeya imemhukumu kifungo cha Miaka 30 jela Mkazi wa Isanga
Jijini Mbeya, Hamad Yusufu, kwa kosa la Kuzini na Binti yake na Kuzaa
naye mtoto mmoja wa Kike.
Baba
huyo anadaiwa kuanza kuzini na binti yake mwaka 2008 akiwa na umri wa
miaka 11 akimtisha kwa kutumia panga na kumpa ujauzito miaka mitano
baadaye na kusababisha akatishe masomo ya elimu ya msingi.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Gilbert Ndeuruo, amesema
Mahakama imezingatia zaidi ushahidi uliotolewa na mtoto wa mshitakiwa
huyo, Hadija Yusufu, anayedaiwa kuzini na kuzaa naye mtoto mmoja, Eva
Yusufu, aliyethibitisha bila shaka kuwa baba yake alimlazimisha kuzini
naye akimtishia kwa panga kwa zaidi ya miaka minne mfululizo kuanzia
mwaka 2008 hadi mwaka 2012, alipopata ujauzito.
Pia Hakimu
Ndeuruo, amesema mahakama hiyo imeridhika bila shaka kuwa mshtakiwa
Hamad amefanya kosa hilo baada ya vipimo vya vinasaba yaani DNA
vilivyowasilishwa Mahakamani hapo na Afisa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu
wa Serikali, Hadija Said Mwema, kuonesha kuwa mshtakiwa huyo amefanana
na mtoto Eva aliyezaliwa na binti yake Hadija, kwa asilimia 99.9.
Kwa mujibu wa taarifa zilizowasilishwa mahakamani hapo na upande wa
mashtaka, ulioongozwa na Mwendesha Mashtaka Lugano Mwakilasa, mshitakiwa
huyo ameanza kuzini na binti yake mwaka 2008 akiwa darasa la Tano baada
ya kuachana na mkewe, Regina Simon, aliyefunga naye ndoa mwaka 1997
mkoani Mbeya.
Hata hivyo, mshitakiwa huyo ameonesha nia ya
kukata rufaa kupinda adhabu hiyo licha ya kushindwa kuitumia fursa ya
kuomba punguzo la adhabu aliyopewa na Hakimu Ndeuruo, akidai anaiachia
mahakama ifanye itakavyo kwa madai hakufanya kosa hilo bali kesi hiyo
imetokana na chuki alizonazo mke wake, Regina Simon, baada ya kuachana.
Nje ya Mahakama, baadhi ya wananchi wametoa maoni yao kuhusu adhabu hiyo.
Hukumu hiyo ni ya pili kutolewa na Mahakamani hapo katika kipindi cha
Julai mwaka huu kuhusu makosa ya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya
watoto wa kike, ambapo hukumu ya kwanza imetolewa na Hakimu Ndeuruo
Julai Mbili mwaka dhidi ya Mchungaji wa Kanisa la Evangelical Assemblies
of Gog, EAGT, mkoani Mbeya, Daniel Mwasumbi, aliyehukumiwa kifungo cha
miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka na kumpa ujauzito mara mbili
mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Itende mjini hapa, Neema Benson.
CHANZO STAR-TV
Comments
Post a Comment