Dr.Jakaya Mrisho Kikwete Raisi wa Jamuhili ya Muungano wa Tanzania |
Raisi wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania mh. Dr. Jakaya Mrisho kikwete hapo kesho anatarajiwa kuwasili katiak mji wa Biharamulo kwa shughuli ya Kuzindua barabara ya Muleba Ngara kupitia Biharamulo mjini iliyo jengwa kwa kiwango cha rami.
kukamilika kwa barabara hii kumeifanya Biharamulo kufunguka kitaifa na kima taifa kwani hapo kabla wilaya hii ilikuwa imesahaulika kabisa kutokana na kuwa na miundo mbinu ya barabara kuwa siyo ya kuridhisha.
Nikiongea na mmoja wa wakazi wa biharamulo mjini anaye julikana kwa jina la patrick alisema kwa furaha "tunashukuru nasi biharamulo tumekumbukwa kwani tulikuwa tuko kisiwani kutoka na na kuwa na babarabara ya vumbi ambayo ilikua mbovu"
Kukamilika kwa barabara hii kuta leta fursa za kibiashara kwa wakazi wa Biharamulo ambapo wataweza kujikomboa na umasikini wa kutupwa. ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa ukichochewa na ubovu wa miundo mbinu.
Uzinduzi huo utafanyika katika eneo la Ngambo Njiapanda ambapo raisi Dr.Kikwete atazindua barabara hiyo kuanzia majira ya saa 2 kamili asubuhi saa za afrika mashariki.
Comments
Post a Comment