Katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji Wilayani Kakonko,kaimu katibu tawala wa Wilaya Kakonko Bw.Aman Alexander, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Malasa,amewaongoza wananchi wa Kijiji Cha Nyakayenzi kilichopo kata ya Kasuga wilayani Kakonko kupanda miti katika chanzo cha maji Nyakayenzi,leo Tarehe 21,Machi,2023. Akizungumza wakati wa zoezi hilo kaimu katibu tawala Bw.Alexander amewasisitiza viongozi wa vijiji kupitia kamati za maendeleo, kuendelea kuwahamasisha wananchi kupanda miti hasa katika vyanzo vya maji Ili kivilinda vyanzo hivyo Pamoja na kukabiliana na mabadiliko tabia nchi. "Viongozi tushirikiane kupanda miti rafiki katika vyanzo vya maji.. Ili kivitunza vyanzo hivi vya maji ,pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi" Aidha Bw.Alexander amewaomba wananchi kukubali kupokea miradi mbali mbali inayoletwa kutekelezwa katika vijiji vyao na waitunze kwani miradi hiyo ndiyo inayochochea maendeleo yanayokusudiwa na Serikali. Kwa upande mwi...