Katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji Wilayani Kakonko,kaimu katibu tawala wa Wilaya Kakonko Bw.Aman Alexander, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Malasa,amewaongoza wananchi wa Kijiji Cha Nyakayenzi kilichopo kata ya Kasuga wilayani Kakonko kupanda miti katika chanzo cha maji Nyakayenzi,leo Tarehe 21,Machi,2023.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo kaimu katibu tawala Bw.Alexander amewasisitiza viongozi wa vijiji kupitia kamati za maendeleo, kuendelea kuwahamasisha wananchi kupanda miti hasa katika vyanzo vya maji Ili kivilinda vyanzo hivyo Pamoja na kukabiliana na mabadiliko tabia nchi.
"Viongozi tushirikiane kupanda miti rafiki katika vyanzo vya maji.. Ili kivitunza vyanzo hivi vya maji ,pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi"
Aidha Bw.Alexander amewaomba wananchi kukubali kupokea miradi mbali mbali inayoletwa kutekelezwa katika vijiji vyao na waitunze kwani miradi hiyo ndiyo inayochochea maendeleo yanayokusudiwa na Serikali.
Kwa upande mwingine kaimu katibu tawala Bw.Alexander amezindua mradi wa maji katika Kijiji Cha Nyakiyobe kata ya Gwarama,Mradi uliotekelezwa Kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la Danish Refugee Council (DRC) likishirikiana na Wakala wa Maji na usafi wa mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya kakonko
Naye Kaimu mkurugenzi wa RUWASA Wilaya Kakonko Bw.Denis Manji, akisoma taarifa ya utekelezaji mradi huo mbele ya mgeni rasimi, ameeleza mradi huo wenye thamani ya zaidi milioni 336 unatarajia kuhudumia takribani wakazi 3000 wa Kijiji Cha Nyakiyobe na vitongoji vyake, ambapo wananchi watapata huduma ya maji kwa kuchangia shilingi kumi (10) kwa ndoo katika magati yaliyojengwa maeneo hayo.
Akizindua Mradi huo Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Kakonko,Kanali Evance Malasa,Kaimu katibu Tawala wa Wilaya Kakonko Bw.Alexander ameendelea kuwasisitiza wananchi kutunza vyanzo vya maji na miundombinu yake Ili viendelee kuwahudimia Kwa ufanisi na Kwa muda mrefu zaidi.
"Nitoe wito Kwa wana Nyakiyobe, Kwenye vyanzo vya maji Shirikianeni na Serikali za Vijiji kuzuia shughuli za kibinadamu kufanyika maeneo hayo Ili kulinda vyanzo vya maji..." Alisema Bw.Alexander.
"Wananchi ambao mabomba ya maji yanapita maeneo yenu yakiwemo mashamba msiyakate ..
mabomba hayo, ...mabomba hayasababishi mazao yasiote au yataotesha Vitu vingine, hivyo itunzeni miundombinu ya maji" aliongeza Kaimu katibu tawala.
Wiki ya Maji wilayani Kakonko imefikia kilele chake leo tarehe 21,March 2023,Ikiwa na Kauli mbiu "Kuongeza kasi ya mabadiliko katika sekta ya maji kwa maendeleo endelevu ya Uchumi".
Comments
Post a Comment