Maafisa Ugani wilayani kibondo mkoani kigoma , wamesema kwa sasa wataanza kutumia mbinu ya kumfikia mkulima mmoja mmoja ili kuongeza tija katika kilimo na kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo .
Wamesema hayo baada ya kukabidhiwa pikipiki kwa ajili ya kuwawezesha kuwatembelea wakulima na kuwashauri njia na mbinu Bora za kilimo ili kufikia azima ya serikali ya sekta ya kilimo kuchangia asilimia kumi ya pato la Taifa ifikapo 2030.
Wamesema awali walikuwa wakitumia mbinua ya shamba darasa kuwafundisha wakulima kutokana na kukosa usafiri lakini kwa sasa baada ya kuwezeshwa usafiri wataweza kuwatembelea na kumfikia mkulima mmoja mmoja lengo ikiwa ni kuongeza tija katika kilimo.
Mkuu wa wilaya ya Kibondo Kanali Agrey Magwaza amewaagiza Maafisa Ugani hao kuzitumia pikipiki walizopewa kuwafikia wakulima na kwamba serikali itafanya ufuatiliaji kuhakikisha pikipiki hizo zinatoa mchango katika sekta ya kilimo kupitia ushauri wa maafisa ugani kwa wakulima.
Chanzo: Kigoma Press Club
Comments
Post a Comment