Na A .C. Kuzenza-Kibondo
Mkuu wa wilaya Kibondo Kanali Aggrey John Magwaza,amewaasa viongozi toka nchini Burundi, kuendelea kuwaelimisha wananchi kuzingatia na kufuata sheria za nchi Ili kuepuka kukinzana na sheria.
Wito huo umetolewa mapema Jana tarehe 01 March,2023 wakati muendelezo wa vikao vya ujirani mwema kwa kamati za ulinzi na usalama baina ya nchi ya Tanzania na Burundi.
Viongozi hao kutoka nchini Burundi wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Ruyigi, Bi. Tabu Emmerencinne, amemshukuru Mkuu wa Wilaya Kibondo pamoja na kamati ya ulinzi na usalama kwa kuwapokea vizuri na kuwapa ushirikiano pamoja na ukarimu kwa kipindi chote walichokuwepo nchini.
Aidha Ameongeza kwa kusema Kuwa,Ushirikiano na ukarimu huo ndiyo tafsiri halisi ya ujirani mwema miongoni mwa Nchi hizi mbili.
Vilevile Bi.Emmerencinne Ameomba mataifa haya yazidi kushirikiana katika nyanja mbalimbali mathalani nyanja za kiusalama kupitia vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea kubadilishana taarifa za kiharifu Ili kuweza kupunguza na hatimaye kumaliza kabisa matukio ya uharifu ndani ya mataifa haya.
Viongozi hao wa Burundi wapo nchini Tanzania kuhudhuria vikao vya ujirani mwema vya kamati za ulinzi na Usalama za Nchi zote mbili vinavyo endelea wilayani Kibondo.
Comments
Post a Comment