Skip to main content

USISEME HAYANIHUSU....

 


Watu wengi Katika Jamii Huwa hawajishugulishi na Jambo lolote Ikiwa tu limetokea Katika Jamii naJambo hilo kuonekana kutowagusa Moja kwa Moja.

Hali hii Mara Zote hutegemea na tabaka la Jamii,mtu/Watu, Imani na pengine Mazingira Jamii iliyopo,Ikilinganishwa na Jambo husika lililotokea.

Wakati nikiwa Mdogo baba na mama yangu walikua wakinieleza Tena kwa vitendo juu ya dhana hii ya kujisemea HAYANIHUSU,Kuna Siku nlikua nikitembea na baba kuelekea shambani Mara njiani  tukakuta Mti Mdogo umeanguka njiani nilifika na kuvuka lakini Baba Yangu Akaniita na kunambia hii si Tabia njema,Maana Njia hii inatumiwa na Watu wengi ndiyo tutakayo tumia kurudi Nyumbani,Na Hatujui tutarudi Kukiwa bado na mwangaza au Usiku ukiwa umeingia, Mti Huu waweza kumuumiza mmoja wetu au watumiaji wengine wa Njia hii... Ukiutoa na Kuweka kando utaonesha kuwa Unawajali na wengine. nikapata Funzo na tangu Siku hiyo  Nikajikuta nikikuta kitu Njiani kinacho weza Leta Madhara kwangu na Watu wengine siwez kukiacha na siwez sema hakinihusu.

Mama yangu Naye Siku moja kuhakikisha kijana wake  si mtu wa kujisemea HAYANIHUSU aliweka masufuria Katika mlango wa chumba changu,wakati Natoka chumbani nikayaruka Wala Siku yatoa na kuyaweka sehemu yanapo paswa kuwekwa..Ilikua kimbembe kwangu kwani mama aliniuliza Umeona masufuria Hayo yapo sehemu sahihi??..nikajifunza  Tena Kumbe Jambo Kama linatokea na unajua sio sahihi na hujafanya jitihada kulisahihisha Ni Makosa.

Hata kwenye Biblia Takatifu Kuna maonyo juu ya Tabia hii ya HAYANIHUSU,Ukisoma Kitabu cha Ezekieli 3:18-19 unaona Mungu anaitolea hukumu Tabia hii ya Kujifanya HAYANIHUSU Unaona mtu Anatenda ubaya na wewe Unaweza kumuonya aache ubaya na Njia zake na humuonyi ikitokea akafa Katika uovu Ule wewe uliyekuwa na uwezo wa kumuonya Damu yake itatakiwa mikononi mwako.

Kifupi Kitendo Cha Kujifanya HAYANIHUSU Ni Hatari Sana Maana Yako Mambo kwa macho ya kawaida Unaweza ona hayakuhusu Lakini kulingana na mahali ulipo,Cheo chako, au nafasi Yako Katika Jamii  kiuhalisia kuna Madhara yatakukuta Hata Kama si kwa wakati huo.

Kuna kisa kingine Katika Biblia kinasimulia juu ya binti wa kabila moja aliyeolewa na mfalme na kuishi Katika Kasri la mfalme,Naye mmoja Kati ya wasaidizi wa mfalme akapitisha Sheria ya kuwaua Watu Wa kabila la binti Yule,Yule binti Awali Akiona Sheria Ile haimuhusu Sababu alikua na uhakika wa ulinzi na kila Kitu Kutoka kwa mfalme,hivyo haikumsubua Kitu Sheria Ile, Hadi alipokuja kuamibiwa na mmoja wa Watu Wa kabila lake kuwa Sheria Ile Hata Yeye inamuhusu na Yeye Ni Miongoni mwa Watu waliotajwa kuangamizwa na Sheria Ile.Lakini kutokana na mazingira ya kuishi Katika Kasri la mfalme  Aliona Kama halimuhusu Moja kwa Moja, Habari hii imeelezwa Katika Kitabu Cha Esta Ile Sura ya 4.

Visa hivi vitufundishe kuwa Haijalishi Mazingira tuliyopo,Cheo,Jamii,Hali ya Uchumi,Elimu, na Sababu zingine tulizonazo kupuuza Mambo na kuona Kama hayatuhusu,Tuyatazame Mambo kwa umakini yamkini yakiwa na kasoro ndani yake tuzisemee Tusiishie Kusema HAYANIHUSU,Maana yataenda yaendako yakifika Mwisho yataturudia Hata sisi tulioyaona hayatuhusu. Tujifunze kwa kisa cha Panya na  Mkulima, aliyevuna mazao na Kuweka mtego Kwaajiri ya kumnasa Panya aliyeanza kuharibu Mazao ya mkulima,Panya Alipo ona mtego Akamfuata Kuku wa mkulima akamwambia nisaidie kuutegua mtego usininase Kuku akasema mtego haunihusu Mimi unakuhusu wewe Panya,Panya kwa masikitiko akaondoka Akamfuata Mbuzi,akamueleza amsaidie kuutegua Mtego Mbuzi akasema mtego ni kwaajiri ya panya haumuhusu Mbuzi,Panya kasikitika Sana Akamfuata Ngombe Naye Akatoa Majibu Kama ya Kuku na Mbuzi, Panya akasikitika Sana na akaenda zake KWA Huzuni na kuomboleza...Siku Moja Nyoka akawa anamuwinda Panya bahati mbaya akapita Eneo la mtego Nyoka akanaswa na mtego,Mke wa mkulima Alikua karibu na mtego, akajua mtego wake umenasa Panya.. Lahaula Kumbe Ni Nyoka!!!! pasi na Kujua Akanyoosha Mkono wake kututoa mtego, na mara Nyoka akamgonga mke wa mkulima. Mkulima Yule akampeleka hospitali mke wake,Katika kumhudumia mke wa mkulima alikaa muda Mrefu hospitalini na mkulima akakosa kitoweo Kwaajiri ya Mgonjwa akaamua kumchinja Kuku Kwaajiri ya kitoweo,Baada ya Muda Kupita mkulima alipokea wageni Kwaajiri ya kumuuguza mkewe,akaona Ni vvyema amchinje Mbuzi Ili wageni wapate kitoweo,Siku zikapita Mke wa mkulima Akafariki Dunia,Waombolezaji Nyumbani kwa mkulima wakawa wengi mkulima akaamua Kumchinja Ngombe Kwaajiri ya kitoweo Wakati Wa Maombolezo na Msiba.

Matukio Haya Yote ya kuchinjwa kwa Kuku,Mbuzi na Ngombe yasingetokea Kama wasingelimwambia Panya Kuwa mtego Ule alotegewa ulikua hauwahusu.wangefanya Jambo Hali isingekuwa hivyo Lakini Walisema mtego ni kwaajiri ya panya na wao Hauwahusu. ... na badaye KWA Namna ya Ajabu mtego Uliwahusu...

Tusiseme Hayatuhusu,Tujitahidi kuchunguza Mambo na kujishughulisha nayo tukiamini Yanatuhusu Kwa Namna Moja ama nyingine. wale wasomaji wa Biblia wanajua Kuwa imetupasa kuchukuliana mizigo Ili Maisha  ya hapa Duniani yaende Ili kumpendeza Mungu na wanadamu *Galatia 6:2a*

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE.

 “MANENO PINGAMIZI YASIKWAMISHE UAMSHO WAKO BINAFSI” (2) Siku ya Pili 28, Aprili 2022  Semina ya Neno la Mungu - Dodoma LINK YA SOMO LA HILI YOUTUBE 👉🏼 https://youtu.be/Rwo70MEHQd0    NAMBA ZA KUTUMA SADAKA, MAOMBI NA SHUHUDA 👉🏼https://bit.ly/Sadaka-Maombi-Shuhuda  UTANGULIZI LENGO YA SOMO ➖Uamsho kutoka kwa Mungu uliokusudiwa kwa ajili yako uweze kuupata majira haya nyakati hizi. Wasomaji wa Biblia, historia ya ulimwengu na kanisa wanajua kabisa kipindi chochote kinachotangulia matatizo, kinachofuata ni maombi na baadaye unafuata uamsho. Kama kuna tatizo limepita katika taifa, ujue kuwa kuna watu watainuka kuomba kwa ajili ya lile taifa, na matokeo yake ni uamsho katika lile taifa. Hili lipo katika kanisa, familia na mahali pengine popote. Msisitizo wa somo hili ni ujue namna ya kufanya wakati Mungu anaachilia uamsho huu katika nyakati hizi, maneno pingamizi yasiwe kikwazo kwako. Pia ujue kitu cha kufanya katika kupokea uamsho huu. Uamsho unaanza na mtu bin...

7 BUSINESS LOCATION THAT INCREASE BRAND VISIBILITY

Marketing has changed and it has become more personal. People nowadays need convenience and you cannot expect that your customer will come to you. You will have to go to your customer again and again so that he does not switch to any other brand. Remember that your customer has numerous options in his hand. Thus your business needs to present in locations where the customer can make his buying decision easily. This is where your business location plays an important role. The process of managing a business is continually changing but more importantly with the advent of online marketing, your business location itself has changed. Because of the increasing usage of internet, Smart phones too are the latest trend and hence the reach of internet is now quadrupled. But it is not necessary that your customer be present only on the internet. Brick businesses are as alive today as online businesses. Below you will find a list of 7 business locations that you should be ...

GET TO KNOW EXTENDED MARKERTING MIX

The extended marketing mix is, as the name suggests, an extension of the marketing mix which was traditionally for products. The 4P’s are also known as product marketing mix. As services came more into the picture it was seen that the 4p’s could not justify the marketing mix. There were 3 more elements which were necessary to actually explain the marketing of services. When products began offering services, the extended marketing mix began applying to products as well (like Maruti service stations where Maruti is a product and the service station is a service). These are the elements which were added to the marketing mix to form the extended marketing mix. In the above figure, the product marketing mix are the first four P’s and the next 3 P’s are added to make the Extended Marketing mix. This extended marketing mix is also known as the service marketing mix. The four PS mainly constituted the following 4 elements Product Price Place Prom...