Watu wengi Katika Jamii Huwa hawajishugulishi na Jambo lolote Ikiwa tu limetokea Katika Jamii naJambo hilo kuonekana kutowagusa Moja kwa Moja.
Hali hii Mara Zote hutegemea na tabaka la Jamii,mtu/Watu, Imani na pengine Mazingira Jamii iliyopo,Ikilinganishwa na Jambo husika lililotokea.
Wakati nikiwa Mdogo baba na mama yangu walikua wakinieleza Tena kwa vitendo juu ya dhana hii ya kujisemea HAYANIHUSU,Kuna Siku nlikua nikitembea na baba kuelekea shambani Mara njiani tukakuta Mti Mdogo umeanguka njiani nilifika na kuvuka lakini Baba Yangu Akaniita na kunambia hii si Tabia njema,Maana Njia hii inatumiwa na Watu wengi ndiyo tutakayo tumia kurudi Nyumbani,Na Hatujui tutarudi Kukiwa bado na mwangaza au Usiku ukiwa umeingia, Mti Huu waweza kumuumiza mmoja wetu au watumiaji wengine wa Njia hii... Ukiutoa na Kuweka kando utaonesha kuwa Unawajali na wengine. nikapata Funzo na tangu Siku hiyo Nikajikuta nikikuta kitu Njiani kinacho weza Leta Madhara kwangu na Watu wengine siwez kukiacha na siwez sema hakinihusu.
Mama yangu Naye Siku moja kuhakikisha kijana wake si mtu wa kujisemea HAYANIHUSU aliweka masufuria Katika mlango wa chumba changu,wakati Natoka chumbani nikayaruka Wala Siku yatoa na kuyaweka sehemu yanapo paswa kuwekwa..Ilikua kimbembe kwangu kwani mama aliniuliza Umeona masufuria Hayo yapo sehemu sahihi??..nikajifunza Tena Kumbe Jambo Kama linatokea na unajua sio sahihi na hujafanya jitihada kulisahihisha Ni Makosa.
Hata kwenye Biblia Takatifu Kuna maonyo juu ya Tabia hii ya HAYANIHUSU,Ukisoma Kitabu cha Ezekieli 3:18-19 unaona Mungu anaitolea hukumu Tabia hii ya Kujifanya HAYANIHUSU Unaona mtu Anatenda ubaya na wewe Unaweza kumuonya aache ubaya na Njia zake na humuonyi ikitokea akafa Katika uovu Ule wewe uliyekuwa na uwezo wa kumuonya Damu yake itatakiwa mikononi mwako.
Kifupi Kitendo Cha Kujifanya HAYANIHUSU Ni Hatari Sana Maana Yako Mambo kwa macho ya kawaida Unaweza ona hayakuhusu Lakini kulingana na mahali ulipo,Cheo chako, au nafasi Yako Katika Jamii kiuhalisia kuna Madhara yatakukuta Hata Kama si kwa wakati huo.
Kuna kisa kingine Katika Biblia kinasimulia juu ya binti wa kabila moja aliyeolewa na mfalme na kuishi Katika Kasri la mfalme,Naye mmoja Kati ya wasaidizi wa mfalme akapitisha Sheria ya kuwaua Watu Wa kabila la binti Yule,Yule binti Awali Akiona Sheria Ile haimuhusu Sababu alikua na uhakika wa ulinzi na kila Kitu Kutoka kwa mfalme,hivyo haikumsubua Kitu Sheria Ile, Hadi alipokuja kuamibiwa na mmoja wa Watu Wa kabila lake kuwa Sheria Ile Hata Yeye inamuhusu na Yeye Ni Miongoni mwa Watu waliotajwa kuangamizwa na Sheria Ile.Lakini kutokana na mazingira ya kuishi Katika Kasri la mfalme Aliona Kama halimuhusu Moja kwa Moja, Habari hii imeelezwa Katika Kitabu Cha Esta Ile Sura ya 4.
Visa hivi vitufundishe kuwa Haijalishi Mazingira tuliyopo,Cheo,Jamii,Hali ya Uchumi,Elimu, na Sababu zingine tulizonazo kupuuza Mambo na kuona Kama hayatuhusu,Tuyatazame Mambo kwa umakini yamkini yakiwa na kasoro ndani yake tuzisemee Tusiishie Kusema HAYANIHUSU,Maana yataenda yaendako yakifika Mwisho yataturudia Hata sisi tulioyaona hayatuhusu. Tujifunze kwa kisa cha Panya na Mkulima, aliyevuna mazao na Kuweka mtego Kwaajiri ya kumnasa Panya aliyeanza kuharibu Mazao ya mkulima,Panya Alipo ona mtego Akamfuata Kuku wa mkulima akamwambia nisaidie kuutegua mtego usininase Kuku akasema mtego haunihusu Mimi unakuhusu wewe Panya,Panya kwa masikitiko akaondoka Akamfuata Mbuzi,akamueleza amsaidie kuutegua Mtego Mbuzi akasema mtego ni kwaajiri ya panya haumuhusu Mbuzi,Panya kasikitika Sana Akamfuata Ngombe Naye Akatoa Majibu Kama ya Kuku na Mbuzi, Panya akasikitika Sana na akaenda zake KWA Huzuni na kuomboleza...Siku Moja Nyoka akawa anamuwinda Panya bahati mbaya akapita Eneo la mtego Nyoka akanaswa na mtego,Mke wa mkulima Alikua karibu na mtego, akajua mtego wake umenasa Panya.. Lahaula Kumbe Ni Nyoka!!!! pasi na Kujua Akanyoosha Mkono wake kututoa mtego, na mara Nyoka akamgonga mke wa mkulima. Mkulima Yule akampeleka hospitali mke wake,Katika kumhudumia mke wa mkulima alikaa muda Mrefu hospitalini na mkulima akakosa kitoweo Kwaajiri ya Mgonjwa akaamua kumchinja Kuku Kwaajiri ya kitoweo,Baada ya Muda Kupita mkulima alipokea wageni Kwaajiri ya kumuuguza mkewe,akaona Ni vvyema amchinje Mbuzi Ili wageni wapate kitoweo,Siku zikapita Mke wa mkulima Akafariki Dunia,Waombolezaji Nyumbani kwa mkulima wakawa wengi mkulima akaamua Kumchinja Ngombe Kwaajiri ya kitoweo Wakati Wa Maombolezo na Msiba.
Matukio Haya Yote ya kuchinjwa kwa Kuku,Mbuzi na Ngombe yasingetokea Kama wasingelimwambia Panya Kuwa mtego Ule alotegewa ulikua hauwahusu.wangefanya Jambo Hali isingekuwa hivyo Lakini Walisema mtego ni kwaajiri ya panya na wao Hauwahusu. ... na badaye KWA Namna ya Ajabu mtego Uliwahusu...
Tusiseme Hayatuhusu,Tujitahidi kuchunguza Mambo na kujishughulisha nayo tukiamini Yanatuhusu Kwa Namna Moja ama nyingine. wale wasomaji wa Biblia wanajua Kuwa imetupasa kuchukuliana mizigo Ili Maisha ya hapa Duniani yaende Ili kumpendeza Mungu na wanadamu *Galatia 6:2a*
Keep stone Rolling
ReplyDelete