Skip to main content

MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE.

 “MANENO PINGAMIZI YASIKWAMISHE UAMSHO WAKO BINAFSI” (2)



Siku ya Pili 28, Aprili 2022 

Semina ya Neno la Mungu - Dodoma


LINK YA SOMO LA HILI YOUTUBE 👉🏼https://youtu.be/Rwo70MEHQd0  


NAMBA ZA KUTUMA SADAKA, MAOMBI NA SHUHUDA

👉🏼https://bit.ly/Sadaka-Maombi-Shuhuda 


UTANGULIZI

LENGO YA SOMO

➖Uamsho kutoka kwa Mungu uliokusudiwa kwa ajili yako uweze kuupata majira haya nyakati hizi.


Wasomaji wa Biblia, historia ya ulimwengu na kanisa wanajua kabisa kipindi chochote kinachotangulia matatizo, kinachofuata ni maombi na baadaye unafuata uamsho.


Kama kuna tatizo limepita katika taifa, ujue kuwa kuna watu watainuka kuomba kwa ajili ya lile taifa, na matokeo yake ni uamsho katika lile taifa. Hili lipo katika kanisa, familia na mahali pengine popote.


Msisitizo wa somo hili ni ujue namna ya kufanya wakati Mungu anaachilia uamsho huu katika nyakati hizi, maneno pingamizi yasiwe kikwazo kwako. Pia ujue kitu cha kufanya katika kupokea uamsho huu.


Uamsho unaanza na mtu binafsi, na sio kikundi. Katika kipindi kilichopita tulitazama uhusiano wa uamsho wako wa leo na mafanikio yako ya kesho. Na tuliangalia habari za kufungwa kwa Petro  baada ya  Yakobo kuuawa.


Matendo ya mitume 12:1-7

Hapa tuliona kuwa katika majira ambayo Petro alikamatwa yalikuwa ni majira ya Pasaka ambayo katika Biblia walisema ni siku ya mikate isiyotiwa chachu.


Herode alikuwa anakifanya wakati wa sikukuu ili wayahudi waendelee kukaa upande wake. Kwa hiyo alimuweka Petro gerezani alindwe na vikosi  vinne vya Askari wanne wanne. 


Mstari wa 5 unasema 5 Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake.


Lile neno juhudi ndani yake lina vitu kadhaa. Vitu viwili ambavyo nimeviona ni :- 


➖Ni vigumu sana kuomba kwa juhudi ikiwa kama hutaona kuwa kama Mungu asipoingilia katika tatizo ulilonalo huna msaada. Kwa hiyo ikiwa huna plan B. Yaani plan zote zimefeli na imebaki moja tu ya Mungu kukusaidia. Ukijua hivyo maombi lazima yaje kwa juhudi ili Mungu akutoe katika hali uliyonayo maana huna msaada zaidi ya Mungu. 


➖Ni kujua ya kuwa majibu yana muda wake ili kutoa msaada kwa mtu ambaye unamuombea.  Petro ilikuwa atolewe katika siku ya sikukuu. Walianza kuomba kabla ya sikukuu. Maana walijua ya kwamba ikiwa hawatapa majibu kabla ya sikukuu basi Petro atauawa.


Yesu alipokuwa katika Bustani ya Getsemane, alisikia huzuni ndani yake. Biblia inasema huzuni ya Dunia inaleta mauti na huzuni ya Mungu inaleta toba iletayo ondoleo la dhambi. Maana yake inakufanya ubadilike.


Yesu alimwambia baba yake roho i radhi lakini mwili ni dhaifu. Na alikuwa kabakiza saa chache sana kabla ya msaliti kuja. Maana angechelewa tu kidogo  angekwama. Akina Petro waliambiwa waombe na hawakuomba walilala. Walipokuja kumkamata Yesu  Petro alitoa panga akamkata mtu sikio.


Hii ina maana kama hujakaa kwenye maombi  tatizo lolote utapambama nalo kimwili. Yesu alikuwa na ujasiri wa kuokota sikio na kulirudisha mahali pake. 


Kuna kipindi ambacho  majibu ya maombi yako yanakuwa na thamani kubwa sana kuliko yakija katika kipindi fulani. Maombi ya juhudi yanalenga kuwa huo muda usiishe kabla hujapata majibu ya maombi yako.


Maombi ya juhudi yanalenga kitu kingine cha kusema Mungu naomba unipe usiniache. Mungu katika hili naomba usinikatalie. Biblia inasema Petro alipokuwa kule gerezani hali yake ilikuwa ni mbaya sana maana alikuwa anajua kabisa Yakobo aliuawa pale pale gerezani. Alipoteza tumaini ndani yake.


Kitu cha Kwanza kilichoingia gerezani baada ya malaika kuangazia ilikuwa ni nuru ikiwa ni ishara ya tumaini kuja. Taifa likipita mahali pagumu linapoteza tumaini. Mungu akianza kujibu anaanza kwa kuleta tumaini katikati ya shida waliyonayo watu.


Kitu cha Pili ni kuachilia na kukurudishia neema ambayo Mungu anakupa katika tatizo ili uweze kutii kile kitu ambacho Mungu anasema na wewe kwa ajili ya kesho yako.


Kesho yako inatengenezwa na leo yako.


  Ukiona unakwamishwa leo basi ujue kuwa kuna kitu ambacho Mungu amekikusudia mbele yako ni kizuri. Kwa sababu hiyo shetani anapigana sana leo kwa sababu ya kesho.


Watu wote waliopita mahali pagumu wanajua ya kwamba kumtii Mungu wakati wa magumu ni ngumu sana. Maana ni sauti ya mazingira inakuwa ni kubwa sana kuliko sauti ya Mungu kwa sababu yanapiga kelele.


Watu na mazingira hayo yanakuwa kama yale ya rafiki zake Ayubu ambao walienda kwake kumfariji. Ayubu aliwaita marafiki wataabishaji. Roho ya uamsho ikija ndani yako inakufungua masikio ya ndani na kukujulisha ya kuwa uwe na tumaini kwa Bwana.  Katikati ya maumivu makali uweze kumsikia Mungu anapokusemesha.


Mstari wa 8 Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate.


Jana tuliacha kile kipengele  cha kwamba ukanifuate. Malaika anamwambia ukanifuate, kwenda wapi? Ukifuatilia ule mstari wa 9 unasema __akatoka nje akamfuata wala hakujua ni kweli yaliyofanywa na malaika bali alidhani kwamba anaona maono. 


Ni ngumu sana mtu ambaye amefungwa ndani ya gereza halafu anatokea malaika anamwambia nifuate halafu milango yote imefungwa. Si kila mtu aliyefunguliwa minyororo yake ametoka gerezani. Petro pamoja na kwamba minyororo ilikuwa imefunguliwa lakini alikuwa bado hajatoka gerezani.


Watu wengi wanafurahia muujiza ambao bado ni kidogo na ndio maana maombi ya uamsho hayawezi kuwa ya siku chache kwa sababu yanasukuma mpaka ufike mahali Mungu anapotaka. 


Mungu hana nia ya kukufungua minyororo halafu ubaki jela kwa sababu sio wote wanaokaa jela wana pingu. Ile kwamba miguu na mikono yako inafanya kazi haina maana hauko gerezani.


Kitu alichokuwa anatafuta ndani yake ni ili afanye maamuzi ndani yake ya kwamba sitabaki katika mazingira nilivyonayo (i'm ready to move) sitakaa katika mazingira niliyonayo kwa sababu Mungu hawezi kumsaidia mtu ambaye ndani yake hajaamua kumfuata, ujikane nafsi yako, ujitwike msalaba wako. 


Nilikuwa nasoma ushuhuda wa mtumishi moja kule Marekani jinsi ambavyo alikuwa anaombea wagonjwa wanapona akaenda kwa mmoja akamwekea mikono akamwambia katika jina la Yesu Kristo simama utembee. Nguvu za Mungu zilikuja na kumnyanyua huyu mtu kutoka kwenye wheel chair akaja hapa juu halafu akamwambia tembea akarudi kwenye wheel chair akasema No nguvu zile zikamwachia akabaki kilema. 


Yule mhubiri akamuuliza kwa nini hukupokea zile nguvu zilizokuja akasema "Nitakosa msaada wa serikali wanaopatiwa wenye shida ya kutembea". Si kila mtu anapenda kuondoka gerezani maana yawezekana gerezani unapata chakula kuliko uraiani.


Mungu akiamua kukusaidia ni lazima uwe tayari ndani yako kwamba ni lazima tutoke hapa. Taifa likiwa limechoka na hali fulani lazima liamue kwamba hali hii enough is enough lazima tusonge mbele. Kama ni suala ndani ya kanisa mnataka kuona mabadiliko ni lazima ndani ya kanisa kuwe na mioyo inayosema Mungu hatutaki tena kukaa hapa tumezunguka mlima huu yatosha sasa tunataka kusonga mbele.


Petro haikuwa  mara ya kwanza kufanya jambo hili alikutwa akivua samaki na asubuhi amekosa samaki na alikuwa anaosha zile nyavu tayari kwa ajili ya kurudi tena jioni. Yesu akaja akaomba ile boti aitumie kuchapa injili halafu baada ya kuhubiri akamuuliza umepata kitoweo leo akasema hatujapata kitu akasema shusha nyavu. 


Mazingira ya kawaida yanamkatalia mzoefu kushusha nyavu angekuwa Kilindini angeshusha nyavu lakini huku karibu na ufukwe unatafuta samaki uzoefu wa ufukwe ulikuwa unakataa lakini wakati Yesu akifundisha watu Petro alikuwa akishikilia boti kwa hiyo maneno alikuwa anayasikia na akamwambia tumetaabika sana. Kwa jinsi ya kawaida nisingeteremsha lakini kwa neno lako nasusha nyavu maana yake alikuwa anawaambia haijalishi mazingira yaliyoko neno lako litanifanya nichukue hatua unayotaka.


Kwa hiyo alipokutana na mazingira hayo gerezani hakikumsumbua anafikiri ni ndoto tu anafikiri ni maono tu hadhani kama ni kitu sahihi lakini amesikia tu nifuate milango yote imefungwa maana yake lazima ujione uko mahali Mungu anataka kabla Hujatoka mahali ulipo. 


Hiyo ndiyo imani.


Imani inaona mahali unapoelekea mahali unapoanzia safari unaona mwisho wa safari kabla hujaanza safari, unaona tumaini la kusonga mbele si kwa sababu unatembea lakini ni kwa sababu ya kitu ulichokiona mbele kwamba ukitembea utakutana nacho kitaweka msukumo ndani yako.


SABABU YA TATU YA UAMSHO

KUKUVUSHA KWENYE MALANGO YALIYO VIZUIZI VIZUIAVYO KESHO YAKO


Matendo 12:9

Biblia inasemaAkatoka nje, akamfuata; na ukisoma ule mstari wa 10 Biblia inasema Na walipopita lindo la kwanza na la pili sasa ule mstari wa 9 alitoka nje ipi wakati walikuwa bado gerezani? Haikuwa nje ya gereza ilikuwa nje ya mtazamo wake kifikra (you have to think outside the box). Kama unataka Mungu akusaidie utoke mahali ulipo lazima ujifunze kufikiri nje ya kibox kilichokufunika mawazo yako. 


Maana aonavyo mtu nafsini mwake, afikirivyo nafsini mwake ndivyo alivyo. Kabla Mungu hajakutoa mahali ulipo, kabla Mungu hajaweka wazo jipya ndani yako kitu anachofanya ni kupangua lango la kwanza  ambalo linazuia mawazo na maamuzi yako.


Lango la kwanza ambalo Mungu anapigana nalo ni fikra na mtazamo. Wakati Yesu anahubiri kwamba tubuni kwa maana ufalme wa Mungu umekaribia alikuwa anasema repent! Maana yake change the way you think. Badili mtazamo wako kwa sababu kuna mtazamo mpya na fikra mpya, kuna mawazo mapya nuru mpya ambayo inakuja. 


Kwa sababu huwezi kufikiri leo kama utakavyofikiri kesho halafu utegemee mabadiliko. Lazima ibadilike namna ya kufikiri ili uweze kubadilika namna ya kuishi na kitu alichokuwa anapambana na Petro cha kwanza kabisa ni lango la fikra zake.


Watu wanaokaa pamoja mara nyingi wanafikiri kwa kufanana na watu wenye mawazo yanayofanana uwe na uhakika wataishi kwa kushirikiana watalindana watakuwa na usemi mmoja. Wanakuwa na mitazamo inayofanana lakini kwanza kwenye fikra.


Kwa hiyo alipokuwa anampitisha kwenye lindo la kwanza Petro alikuwa kwenye geti ya pili kwa sababu lile geti la kwanza na la pili kwa Petro lilikuwa ni lango la tatu kwa kuwa lango la kwanza ni lile lilokuwa limefunga kufikiri kwake.


Kuna watu ambao wanajua kabisa mahali wanapopita si sawa,  na Mungu anawaletea mawazo mapya halafu kila wakati wanawaza ndani yao watu watawaonaje? Na wanabaki walipo.


Lazima utoke hapo, hilo ni lango lako la kwanza,  la pili ni lile ambalo ni la geti kulikuwa na askari. Ili ufahamu ya kwamba katika kila geti Mungu analokupitisha kuna askari maana yake kuna watu ambao wasingetaka uvuke hapo.


Na ukishavuka hapo unakutana na mtu anakusemesha maneno magumu sana, usipojua namna ya kuwapisha hao watu utakwama.  Kuna watu kila kona wanaotafuta mbaki wote mlipokwama. Msalaba sio wa kikundi ni wa kila aaminiye. 


Ukisoma habari ya wale wajenzi wa Mnara wa Babeli walikuwa na lugha na usemi mmoja na walikusudia kujenga mnara mpaka mbinguni. Mungu akaamua kuwachafua usemi na lugha zao. Kuchafua lugha na usemi wa watu maana yake ni kumuwekea mawazo tofauti na wenzake kwenye group.


Ni muhimu sana ujue hili kwa sababu kuna watu ndani ya gereza wasingetaka utoke.


USHUHUDA 

Kuna vitu tulikuwa tunakutana navyo kipindi kile ndio tunaokoka na hatukuvipenda. Maisha ya wokovu hayakuwa mepesi lakini tunachuchumilia mbele.


Lakini kuna vitu tulifanya maamuzi na mke wangu kwamba kwetu sisi hapana/no, japo tulikuwa tunavikuta katikati ya watu waliookoka.


Isaya 55:8-9

"Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu."


Angalia 


ISAYA 56:12

"Husema, Njoni, nitaleta divai, Na tunywe sana kileo; Na kesho itakuwa kama leo, Sikukuu kupita kiasi."


Kuna watu ambao wanataka kesho iwe kama leo wakati sisi hatutaki leo yetu ifanane na kesho yetu, tunataka kutoka utukufu kwenda utukufu, imani kwenda imani. Lakini lazima liingie neno jipya ndani yako ambalo litapingana na mazingira ya kawaida.


Katikati ya uamsho kunakuwa na vita kubwa kuliko unavyofikiri na inatokana na mazingira unayokuwa nayo.


USHUHUDA 

Nilikuwa nafundisha umuhimu wa kutoa fungu la kumi kwenye kanisa moja.


Na kulikuwa na wamisionary wengi kanisani, nilifundisha kwa muda mredu kidogo. Baada ya wiki mmiosionary mmoja akanipigia simu kunieleza kuwa amepata shida kanisani kwao, amepeleka fungu la kumi wamelikataa wao hawana sadaka ya aina hiyo. 


Akaniuliza ndio nafanyaje? Nikamwambia asome Biblia yake maana, Biblia inasema fungu la kumi ni la Mungu kwa hiyo nikamuambia amuombe Mungu atamuelekeza pa kulipeleka.


Mungu anapoleta kitu kipya kwa ajili ya kukuchukua ulipo usije kufikiri kila mtu atakipokea na kukielewa. Kuna watu wanataka kesho yao ifanane na leo yao kwa sababu tu leo anafurahi, anataka kufurahi kesho kwa kiwango cha leo. Jifunze kuepukana na watu wa aina hiyo.


LANGO LA NNE

Hili tunalipata kwenye Matendo ya Mitume 12. La kwanza atoke kwenye fikra alizokuwa nazo afikirie nje ya box (ya mazingira), la pili utakuta kwenye lindo la kwanza na la tatu lipo kwenye lindo la pili.


Maandiko yanasema "Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hata mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia wenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha"


Kwa hiyo wametoka ndani ya gereza na Malaika akasukumwa na yale maombi wanayoomba kanisani hawakujua mazingira aliyokuwa nayo wakati huo.  Wanachojua ni kwamba ule msukumo wa kuomba bado haujaondoka.


Ilibidi Malaika amtoe nje mpaka mjini ni kwenye kiwango cha juu sana cha kufikiri kwake.


Petro ilibidi atolewe kwenye kufikiri kuliko funga eneo/kijiji/kanisa. Haina  maana tu kuwa anakuchukua kwa jinsi ya mwili, bali anakuchukua kwa jinsi ya fikra ili usiishi sawa sawa na ulipooka.


Lango lile likawafungukia, lakini pale napo kulikuwa na walinzi wanaoweza kumzuia asiende mahali, lakini Malaika walihakikisha wanampitisha Petro salama kiasi kwamba hatuoni kama wapo.


Lile lango la Nne linashughulika vitu vingi sana. Kama upo kwenye kifungo na ukatolewa kifungoni na ukaingia kwenye mji na huku una mawazo yale ya kule ukiwa kifungoni huna msaada. Mungu akikurudisha kwenye mji anakurudisha na wazo jipya ili uwe chachu kwa ajili ya eneo hilo. 


Alipotoka namna hiyo pale nje ndipo anaelewa kuwa kile kitu ni halisi. Huko kote amepita na ufahamu wake haujaguswa kwa namna ya kutambua hali yale na mazingira aliyoko ghafla anagundua. Saa nyingine inachukua muda mrefu kwa baadhi ya watu waliookoka na wasiookoka, kuweza kuunganisha neno la Bwana na uhalisia uliopo (kulitumia neno kwa ajili ya maisha yetu ya kila siku) watu wengi sana wanampenda Mungu kwa sababu ya uponyaji. 


Inamaanisha kama hakuna ugonjwa huna mahusiano na Mungu, huhitaji miujiza - huna mahusiano na Mungu. Na kama mahusiano yako na Mungu yanategemea hicho tu ujue mahusiano hayo yanaweza kuvunjika kirahisi muda wowote kwa sababu msalaba umejengwa juu ya upendo wa Mungu. 


Mungu alitupenda tungali wenye dhambi (tulivyo) na sisi tumpende alivyo; hata kama hajatupatia kitu chochote (ameweka mikono mifukoni) tunatakiwa kumpenda. 


LANGO LA TANO

NI LANGO KWA MARIAMU 

Matendo ya Mitume 12 : 12-14 utaona baada ya kubisha mlango haukufunguliwa. Usije ukafikiri kwa sababu watu wanakuombea wanataka wakufuate ukishatoka. Yaani wamekuombea na umetoka katika kifungo ila wanapata mashaka kama ni wewe kweli umetoka (hawakuamini kama Mungu amejibu haraka sana). 


Kuna mahali unapita ambapo hata viongozi wako, wapendwa na waombaji wenzako wanakaa mbali nawe. Mpaka unaona kama vile kila mtu amekuzira na Mungu anataka urudi katikati yao kwani amekuteremshia nuru ili uwasaidie watu hao. Mungu atakurudisha katikati yao na wao wakufungulie mlango (wakupe kibali) ili wajue kwamba Mungu amejibu. 


Nguvu za uamsho hazikuachi njiani; zitakupeleka kila mahali milango ilipofungwa kwa ajili yako nayo itafunguliwa. 


LANGO LA SITA 

Matendo ya Mitume 12:17

“Naye akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Kampasheni Yakobo na wale ndugu habari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine.”


Hapa kuna lango kwa Mungu kujibu maombi yao kwa kumfungua yaani yuko huru na kupata kibali katikati yao, lakini mahali anapompeleka sio pale.


Wapendwa wengi sana wanaishia kufurahia muujiza - hawaangalii kesho yao. 


Biblia inasema wasifurahi kwa sababu mapepo yanawatii bali kuna kesho yake. Sio kwamba Mungu anakataa kusifiwa bali majibu ya maombi yenu ni lango tu la kutokea. Usiishie kushukuru wakati umebaki hapo langoni ukipiga nyimbo na kushukuru; amekufungua ili uchukue hatua nyingine ya kusonga mbele. 


Mungu hawezi akakutoa magerezani halafu ukae tu usiwe na kazi, lazima akakutoa hapo na kukupeleka kwingine kwa sababu kuna wapendwa hawaangalii juu ya kesho yako bali wanafurahi kupata vazi jeupe na wanashikilia lisichafuke. 


Ukiingia kazini kuna muda litachafuka au litachanika-chanika ila uwe na uhakika Bwana atakupa vazi jipya. Sasa wengi sana wamebaki kituoni wakisubiri kunyakuliwa. Bwana alitukomboa tufanye kazi. 


Petro alitolewa pale kwa sababu kile kikosi cha maombi kilimsaidia kwa maombi ila kinamkwamisha kimaisha. Kwa hiyo unaona Petro alipita milango yote sita na kote alipita kwa kusukumwa na maombi na Mungu hajawaacha kuomba kwa sababu hajamfikisha mahali ambapo yuko huru. 


Lazaro alipotoka kaburini alitoka na nguvu zote na sauti ya Mungu, lakini nguvu hizo hazikumtoa sanda mikononi na miguuni. Hii ni kwa sababu kuna sehemu kanisa linatakiwa lifanye kwa ajili ya kesho ya Lazaro. 


Kuna kipato unatakiwa kukipata baada ya kutoka kifungoni sasa wengine mnabaki wote mnapiga tu nyimbo na kama hakuna chakula wanasema mfunge. 


Uamsho ukiingia kuna watu watabaki kufurahia na kubaki kuomba wakasahau kuna kulisha familia na kujenga taifa. 


SABABU YA NNE

KUBADILISHA VIFUNGO VYAKO NA KUKWAMA KWAKO NA KUWA USHUHUDA KWAKO


Kati ya kitu Mungu anakitarajia kwako baada ya uamsho kukufikia ni kuzaliwa kwa shuhuda nyingi sana kwa sababu kila anayeguswa na kukwamuliwa sehemu anapata ushuhuda. 


Huo ushuhuda una kazi mbili kuu kazi ya kwanza ni kuonesha kuwa:


➖ Mungu yuko Hai - kwamba anaweza kukutetea na kukupigania. Usiishie kumwona tu mtumishi bila kumwona Mungu. Kazi ya shuhuda ni kumwinua Kristo (msalaba) ili watu waukimbilie msalaba.


➖ Kuamsha tumaini kati ya watu waliokata tamaa na wanaopita kwenye shida kama ya kwako uliyopita. Utasema ulikuwa vile, Mungu akakutembelea na sasa uko hivi. Uwe na uhakika kuna mtu alikuwa kama wewe jana atatiwa moyo aje awe kama wewe wa leo. 


Unaeleza ushuhuda wa kitu ambacho Mungu amekufanyia Kwa sababu wewe mwenyewe ulikuwa umekataa tamaa, lakini kuna mtu anakutia moyo ili uweze kasonga mbele na kukuambia kuwa inawezekana. Usikate tamaa.


Mungu akikugusa wewe anataka umguse na mwingine ili aweze kujua na kutiwa moyo. Kwa maana hiyo usinyamaze na ushuhuda wako maana hiyo ndio injili yako ya kumtia moyo mtu mwingine.


Unaposoma Biblia unaona sehemu kubwa ni shuhuda za watu ambao Mungu aliwahudumia ili tupate kujua  ya kuwa yuko Mungu aliye Hai ili tupate kumuamini na kupokea uzima wa milele.


Wimbo ..he touched me…


Msalaba ulifanya kitu kikubwa ambacho Dunia nzima iliona kama haiwezekani. Maana ilichukua dhambi zetu na kuzigongomezea pale msalabani na Bwana Yesu akachukua na tukasamewa. Tunaposamehewa  anafuta dhambi zote.


Katika agano la kale kulikuwepo na kumbukumbu la dhambi. Na hili huwa linatesa sana. Maana unasikia kuhukumiwa kila wakati. Na lilikuwa linatesa na mbinguni pia maana lilikuwa linawanyima watu uhuru wa kusimama mbele za Bwana.


Msalaba ulifanya  kitu kikubwa sana ambacho kilionekana hakiwezekani. Kuna wakati unakutana na kijana  anasema hata hajui ya kwamba kafikaje katika semina. Maana alikuwa amekata tamaa kabisa ya maisha na alitaka kujiua.


Lakini anakuja katika semina na Mungu anatoa nafasi ya kuita watu waliokoka na yeye anatoka hapo. Anaokoka na Mungu anabadilisha maisha yake kabisa na anapata tumaini jipya. Ndani yake.


USHUHUDA.

Nilikutana na kijana mmoja anavuta bangi na anafukuzwa kila shule. Nilimuuliza yule kijana kuwa ile habari ya kuvuta bangi na kufukuzwa shule je ni ya kweli? Akasema ndio. Kwa hiyo nikaongea na wazazi wake ili watupishe kidogo niweze kuongea na kijana akiwa peke yake.


Walipotupisha nilianza kuongea na yule kijana.


Yule kijana alisema Mwalimu naomba usije ukanichoka na kunikatia tamaa kama vile wengine walivyonikatia tamaa. Akaniambia hii hali siipendi na najaribu kutoka lakini nashindwa. Nikamwambia yuko Mungu na atakusaidia.


Basi akaniambia habari yake yote.  Nikamuuliza je umewahi kufanya sala ya toba akasema ndio nyingi sana. Nikamwambia sasa utafanya tena. Baada ya kumuongoza sala hiyo  nikampa namba yangu ya simu. Nikamwambia kuwa ukisikia kiu ya kuvuta bangi nipigie simu.


Pia nilimwambia kuwa Mungu ananiambia kuwa kule chumbani kwako umeweka msokoto wa bangi ili uwe unavuta akasema ndio baba. Nikamwambia ukaitoe na kabla hujaingia chumbani kwako nipigie simu tuombe. Halafu nenda moja kwa moja chumbani kwako mahali bangi ipo na itoe.


Hakikuwa kitu rahisi maana katika ratiba uliyonayo, Mungu anakuletea mtu wa kumfuatilia ili na ujue kapiga simu saa ngapi. Niliendelea na yule kijana vizuri akawa anapiga hatua.  Akifika mahali pagumu alikuwa anapiga simu anasema baba nisaidie. Tunaomba na anavuka kabisa.


Nilikutana na mtu mmoja akiwa yuko form six, hata usiku alikuwa anatupigia simu amelewa. Anaaanza kusema baba nimekunywa tena nisaidieni kwa nini ninashindwa? Kwa hiyo tukawa tunaomba naye.


Siku moja alituliiza je kwa nini hamnikatii tamaa? Tukamwambia hatuwezi kukutatia tamaa. Kwa maana Yesu alikufa kwa ajili yako. Baada ya muda alikuja akavuka kabisa.


Maombi ya uamsho huombi mara moja au mbili, unaomba mpaka Mtu kavuka kabisa katika malango yote. Inategemea kafungwaje fungwaje. Kwa hiyo omba Mpaka kavuka mahali pote. Msalaba uliachilia kitu kikubwa sana.


Kuna mtu mmoja alikuja kunieleza habari za ugomvi wake na mke wake. Waligombana sana. Ukiangalia kwa kweli unaona kuna tatizo kwa mke wake. Nikamuuliza tena nikasema je  unataka mke wako aende mbinguni au jehanamu? Akasema mbinguni,  nikamwambia msaidie huyo mama. Akinitazama, akasema ni ngumu sana, nikamwambia ingekuwa rahisi basi msalaba usingekuwepo. 


Msalabani hapo ndipo tunatua mizigo yote na kupata msaada. Najua katika jamii tuna watu ambao wanapita mahali pagumu sana. Ile kwamba wewe hujapita hapo basi usimsaidie mwenzako. Mpeleke msalabani kwa Yesu ili amsaidie.


Maombi: Kwa watu ambao walisema Mungu kwa style hii sioni kama unanipenda tena. Na umefika mahali umezira ndani ya moyo wako. Hata mwingine wokovu ameacha. Mungu anataka akurudishie tena nuru ya wokovu.


Ungana nasi kwa maombi haya siku ya leo pale juu katika link niliyokuwekea juu ya somo hili. Karibu tena siku ya tatu.



Comments

Popular posts from this blog

TISS YAPATA BOSS MPYA.

  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, Amemteua Bw.Said Hussein Masoro kuwa Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa taifa,Kuchukua nafasi ya Kamishina Diwani Athuman Msuya  Ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Kabla ya Uteuzi huo Bw.Masoro alikua akihudumu katika Idara ya Usalama wa Taifa kama Naibu Mkurugenzi mkuu na Mkurugenzi wa shughuli za  ndani wa Usalama wa Taifa. Wakati huo huo Rais Dkt.Samia amemteua Balozi Hussein Othman Katanga Kuwa Balozi wa Tanzania mjini New York, Nchini Marekani na muwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa. Balozi Katanga anachukia nafasi ya Balozi Profesa Kennedy Gaston,Ambaye Uteuzi wake umetenguliwa. Balozi Katanga kabla ya Uteuzi huu alikua Katibu Mkuu Kiongozi. Vile vile Mhe.Rais Dkt.Samia amemteua Bw.Moses Mpogole Kusiluka Kuwa Katibu Mkuu Kiongozi,Ambapo kabla ya Uteuzi huo alikua Katibu Mkuu Ikulu. Taarifa Rasimi Kutoka Kurugenzi ya mawasiliano ya Raisi Ikulu iliyotolewa mapema Jana Januari 3,2023, i...

JESHI LA POLISI LATANGAZA AJIRA KWA MWAKA 2012/2013 KWA WAHITIMU WATARAJIWA WA VYUO

TANGAZO LA AJIRA Jeshi la Polisi Tanzania katika mwaka wa fedha 2013/2014 litaajiri vijana kutoka katika makundi yafuatayo: waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012, kidato cha sita mwaka 2013, JKT/JKU mwaka 2013 na vyuo vya elimu ya juu mwaka 2013. Taratibu zinakamilishwa ili waliomaliza kidato cha nne na sita na waliojaza fomu za maombi kabla ya kumaliza mitihani yao ya mwisho waitwe kwenye usaili. Usaili wa vijana wa JKT umekamilika mapema mwezi Aprili, 2013. Tangazo hili linawaalika vijana walioko kwenye vyuo vya elimu ya juu nchini watakaohitimu masomo hivi karibuni na wanaopenda kujiunga na Jeshi la Polisi kujaza fomu za maombi zinazopatikana kwenye tovuti ya Polisi kwa anuani www.policeforce.go.tz www.policeforce.go.tz Fomu za waombaji baada ya kujazwa kikamilifu ziletwe na mkuu wa chuo kabla ya tarehe 30/6/2013 kwa: Inspekta Jenerali wa Polisi, Makao Makuu ya Polisi, S.L.P. 9141, DAR ES SALAAM . Fani zinazotakiwa ni; Shahada za Menejimenti ...

GET TO KNOW EXTENDED MARKERTING MIX

The extended marketing mix is, as the name suggests, an extension of the marketing mix which was traditionally for products. The 4P’s are also known as product marketing mix. As services came more into the picture it was seen that the 4p’s could not justify the marketing mix. There were 3 more elements which were necessary to actually explain the marketing of services. When products began offering services, the extended marketing mix began applying to products as well (like Maruti service stations where Maruti is a product and the service station is a service). These are the elements which were added to the marketing mix to form the extended marketing mix. In the above figure, the product marketing mix are the first four P’s and the next 3 P’s are added to make the Extended Marketing mix. This extended marketing mix is also known as the service marketing mix. The four PS mainly constituted the following 4 elements Product Price Place Prom...