Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2022

SIMBA CHINI YA MATOLA

  picha KWA Hisani ya MTANDAO wa #Lemutuz Updates# Mabingwa wa Soka Mara Nne mtawalia nchini Tanzania Timu ya Simba Sc Yenye makazi yake Mtaa wa Msimbazi Jijini Dar-es-salaam, Wamefikia Makubaliano ya pande Zote mbili kuachana na Kocha mkuu wa Klabu hiyo  Pablo Franco Martin Leo Mei 31,2022. Taarifa rasimi iliyotolewa na Afisa Mtendaji mkuu wa Klabu Barbara Gonzalezi Inaeleza kuwa Uongozi umefikia Makubaliano ya pande Zote Mbili kuvunja mkataba na Kocha mkuu Pablo Franco Martine. Wakati Huo Huo Taarifa hiyo imeeleza kuwa Uongozi  umefikia Makubaliano kuvunja mkataba wa Kocha wa viungo Daniel de Castro Reyes. Tarifa inaongeza Kuwa kikosi Cha Klabu ya Simba kitakua Chini ya Kocha msaidizi mzawa Suleman MATOLA hadi msimu huu utakapo fikia Tamati. Kocha pablo Tangu Atue Klabuni hapo hapo Mwishoni mwa mwaka Jana 2021 Ameiwezesha Klabu ya Simba Kutwaa kombe la Mapinduzi na kutinga Hatua ya Robo fainali ya Kombe La Shirikisho Barani Afrika, na Kushka Nafsi ya pili Katika msimamo...

YANGA YAMPA MKONO WA KWAHERI NTIBAZONKIZA.

   *Na.Anthonius Kuzenza* Uongozi wa Klabu ya soka ya Yanga Yenye makazi yake Jijini Dar-es-Salaam,Leo Mei 30,2022 imeachana Rasmi na Kiungo wake mshambuliaji Saidi Ntibazonkiza Raia wa Burundi. Taarifa Rasmi iliyotolewa na Klabu hiyo inaelezea Uongozi umefikia Maamuzi Hayo kufuatia Kandarasi ya Mwanandinga huyo maarufu kufikia ukingoni leo Mei 30,2022 Baada ya kuitumikia Klabu hiyo kwa Kandarasi ya miaka miwili. Ntibanzokiza alijiunga na Klabu ya Yanga Kama Mchezaji Huru Katika msimu wa 2020/21 Wakati Wa usajiri Wa Dirisha dogo. Akiitumikia Klabu ya Yanga Ameisaidi kushinda kombe la mapinduzi na hadi Kandarasi yake inafikia Mwisho ameisaidia KWA kiwango kikubwa Timu yake kuongoza ligi ya NBC Ambapo Klabu ya Yanga imebakiza Alana 3 Tu kuwezaa kutangazwa Rasmi Kuwa mabingwa wa ligi kuu NBC Tanzania bara KWA msimu Huu 2021/22 Baada ya kuukosa KWA takribani misimu minne iliyopita. Ntibanzokiza Mara ya Mwisho aliitumikia Timu ya Yanga ilipo cheza Dhidi ya Biashara United ya Mara n...

MJUE SGT RAYMOND:MBUNIFU WA MASHINE YA KUBANGUA CHIKICHI(MISE).

  Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma SACP Chacha Bina(wa pili julia) akiwa na Wakuu wa Magereza yaliyopo Mkoa wa Kigoma  Wakimsikiliza Sgt Raymond ( mwenye koti la bluu)mgunduzi wa Mashine ya kubangua chikichi (Mise). PICHA na Ofisi ya mkuu wa Magereza Mkoa Kigoma.   NA. Anthonius Kuzenza Katika Hali ya kutia Moyo na kuhamasisha ubunifu ndani ya Jeshi la Magereza Askari no B.3527 Sgt Reymond  Wilson  wa Gereza Bangwe Mkoani kigoma, Amebuni Mashine ya kubangua Mbegu za chikichi(Mise) Akizungumza Mbele ya Mkuu Wa Magereza Mkoa Wa Kigoma SACP Chacha Bina, Sgt Raymond anasema Amebuni Mashine hiyo Kwa kuunganisha Injini ya pikipiki Kama chanzo Cha Nguvu ya kuendesha Mashine hiyo kwa kuiboresha Injini hiyo na kuongeza ubunifu wake binafsi. Sgt Raymond anaeleza Kuwa Alipata wazo Hilo baada ya kufanya utafiti na Kugundua Kuwa maeneo Mengi ya mkoa Wa Kigoma Ambako wakulima Wa zao la chikichi wapo hakuna nishati ya uhakika ya umeme, Hivyo kwa akabuni Mashine hii ikiwa Ni mba...

MO:SIMBA BADO IMEFANIKIWA.*

   *Na.Anthonius Clement-Kigoma*  Raisi wa heshima na Muwekezaji wa klabu ya Soka ya Simba Mohamed Dewji, amesema Timu ya Simba bado Ni Timu iliyofanikiwa licha ya Kuwa msimu Huu kutokuwa na Kiwango kizuri Katika mashindano ya Ndani. Mo ameyasema Hayo katika chapisho kwenye ukurasa wake wa kijamii wa mtandao wa Facebook. Sehemu ya Chapisho Hilo inasema ".......Najivunia kuweza kusema tupo Katika orodha ya vilabu Bora 12 Afrika" "Hii imekua Mara ya kwanza Simba Kuwa na muendelezo mzuri katika miaka 86 ya historia Yetu" iliongeza Taarifa hiyo. Hata hivyo Mo Dewji kupitia Taarifa yake hiyo ameandika Kuwa KWA Kipindi Cha miaka mitano iliyopita Simba imekua Katika mafanikio makubwa Katika mashindano ya Ndani na mashindano ya kimataifa KWA kutwaa vikombe vingi  vya mashindano ya Ndani ya nchi,Na kuweza Kuweka alama Katika mashindano ya kimataifa KWA kufika hatua ya Robo fainali Mara Tatu mfululizo Katika mashindano ya klabu bingwa Afrika. Taarifa imeongeza kuwa uongozi ha...