*Na.Anthonius Kuzenza*
Uongozi wa Klabu ya soka ya Yanga Yenye makazi yake Jijini Dar-es-Salaam,Leo Mei 30,2022 imeachana Rasmi na Kiungo wake mshambuliaji Saidi Ntibazonkiza Raia wa Burundi.
Taarifa Rasmi iliyotolewa na Klabu hiyo inaelezea Uongozi umefikia Maamuzi Hayo kufuatia Kandarasi ya Mwanandinga huyo maarufu kufikia ukingoni leo Mei 30,2022 Baada ya kuitumikia Klabu hiyo kwa Kandarasi ya miaka miwili.
Ntibanzokiza alijiunga na Klabu ya Yanga Kama Mchezaji Huru Katika msimu wa 2020/21 Wakati Wa usajiri Wa Dirisha dogo.
Akiitumikia Klabu ya Yanga Ameisaidi kushinda kombe la mapinduzi na hadi Kandarasi yake inafikia Mwisho ameisaidia KWA kiwango kikubwa Timu yake kuongoza ligi ya NBC Ambapo Klabu ya Yanga imebakiza Alana 3 Tu kuwezaa kutangazwa Rasmi Kuwa mabingwa wa ligi kuu NBC Tanzania bara KWA msimu Huu 2021/22 Baada ya kuukosa KWA takribani misimu minne iliyopita.
Ntibanzokiza Mara ya Mwisho aliitumikia Timu ya Yanga ilipo cheza Dhidi ya Biashara United ya Mara na Kutoka sare ya Goli 1-1.
Siku Moja Baada ya Mechi Kati ya Biashara United ya Mara dhidi ya Yanga, Taarifa iliyotolewa na afisa habari wa Klabu ya Yanga Haji Sunday Manara Alikaririwa Akisema Uongozi wa Yanga umewasimamisha Wachezaji Wawili Saidi Ntibanzokiza na Dickson Ambundo KWA Makosa ya Kinidhamu.
Uongozi wa Yanga umemshukuru ntibazonkiza KWA utumishi wake ndani ya Klabu na umemtakia kila la Kheri na mafanikio ya soka nje ya Klabu ya Yanga,imemalizia Taarifa hiyo.
Comments
Post a Comment