*Na.Anthonius Clement-Kigoma*
Raisi wa heshima na Muwekezaji wa klabu ya Soka ya Simba Mohamed Dewji, amesema Timu ya Simba bado Ni Timu iliyofanikiwa licha ya Kuwa msimu Huu kutokuwa na Kiwango kizuri Katika mashindano ya Ndani.
Mo ameyasema Hayo katika chapisho kwenye ukurasa wake wa kijamii wa mtandao wa Facebook.
Sehemu ya Chapisho Hilo inasema ".......Najivunia kuweza kusema tupo Katika orodha ya vilabu Bora 12 Afrika"
"Hii imekua Mara ya kwanza Simba Kuwa na muendelezo mzuri katika miaka 86 ya historia Yetu" iliongeza Taarifa hiyo.
Hata hivyo Mo Dewji kupitia Taarifa yake hiyo ameandika Kuwa KWA Kipindi Cha miaka mitano iliyopita Simba imekua Katika mafanikio makubwa Katika mashindano ya Ndani na mashindano ya kimataifa KWA kutwaa vikombe vingi vya mashindano ya Ndani ya nchi,Na kuweza Kuweka alama Katika mashindano ya kimataifa KWA kufika hatua ya Robo fainali Mara Tatu mfululizo Katika mashindano ya klabu bingwa Afrika. Taarifa imeongeza kuwa uongozi hautarudi nyuma Bali utafanya Kazi maeneo Yenye madhaifu Ili kusonga Mbele na mapambano yaendelee imehitimisha Taarifa hiyo.
Klabu ya Simba Msimu Huu wa Mashindano ya Ligi kuu NBC na mashindano ya kombe la Shirikisho ASFC haijawa na Wakati mzuri,Kwani Hadi Sasa wanashika nafasi ya pili Katika msimamo wa Ligi kuu NBC wakiwa na Alama 53 nyuma ya kinara wa Ligi ya NBC Timu ya Yanga(Young Africans) wenye Alama 63.
Pia Simba iliondoshwa Katika mashindano ya kombe la Shirikisho la Azam ASFC hatua ya Nusu fainali na Mtani wake wa Jadi Yanga Baada ya Kufungwa Bao 1-0 Mchezo uliopigwa Katika uwanja wa CCM kirumba Siku ya Jumamosi Mei 28,2022.
Comments
Post a Comment