picha KWA Hisani ya MTANDAO wa #Lemutuz Updates#
Mabingwa wa Soka Mara Nne mtawalia nchini Tanzania Timu ya Simba Sc Yenye makazi yake Mtaa wa Msimbazi Jijini Dar-es-salaam, Wamefikia Makubaliano ya pande Zote mbili kuachana na Kocha mkuu wa Klabu hiyo Pablo Franco Martin Leo Mei 31,2022.
Taarifa rasimi iliyotolewa na Afisa Mtendaji mkuu wa Klabu Barbara Gonzalezi Inaeleza kuwa Uongozi umefikia Makubaliano ya pande Zote Mbili kuvunja mkataba na Kocha mkuu Pablo Franco Martine.
Wakati Huo Huo Taarifa hiyo imeeleza kuwa Uongozi umefikia Makubaliano kuvunja mkataba wa Kocha wa viungo Daniel de Castro Reyes.
Tarifa inaongeza Kuwa kikosi Cha Klabu ya Simba kitakua Chini ya Kocha msaidizi mzawa Suleman MATOLA hadi msimu huu utakapo fikia Tamati.
Kocha pablo Tangu Atue Klabuni hapo hapo Mwishoni mwa mwaka Jana 2021 Ameiwezesha Klabu ya Simba Kutwaa kombe la Mapinduzi na kutinga Hatua ya Robo fainali ya Kombe La Shirikisho Barani Afrika, na Kushka Nafsi ya pili Katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC,Ikiwa imebaki Michezo minne tu Ligi ya NBC Kufikia Tamati.
Aidhauongozi wa Simba Umewatakia KILA la kheri Kocha mkuu Pablo na Mtaalam wa Viungo Daniel Castro Katika Majukumu Yao,Ilimalizia Taarifa huyo.
Comments
Post a Comment