“MANENO PINGAMIZI YASIKWAMISHE UAMSHO WAKO BINAFSI” (2) Siku ya Pili 28, Aprili 2022 Semina ya Neno la Mungu - Dodoma LINK YA SOMO LA HILI YOUTUBE 👉🏼 https://youtu.be/Rwo70MEHQd0 NAMBA ZA KUTUMA SADAKA, MAOMBI NA SHUHUDA 👉🏼https://bit.ly/Sadaka-Maombi-Shuhuda UTANGULIZI LENGO YA SOMO ➖Uamsho kutoka kwa Mungu uliokusudiwa kwa ajili yako uweze kuupata majira haya nyakati hizi. Wasomaji wa Biblia, historia ya ulimwengu na kanisa wanajua kabisa kipindi chochote kinachotangulia matatizo, kinachofuata ni maombi na baadaye unafuata uamsho. Kama kuna tatizo limepita katika taifa, ujue kuwa kuna watu watainuka kuomba kwa ajili ya lile taifa, na matokeo yake ni uamsho katika lile taifa. Hili lipo katika kanisa, familia na mahali pengine popote. Msisitizo wa somo hili ni ujue namna ya kufanya wakati Mungu anaachilia uamsho huu katika nyakati hizi, maneno pingamizi yasiwe kikwazo kwako. Pia ujue kitu cha kufanya katika kupokea uamsho huu. Uamsho unaanza na mtu bin...