Skip to main content

1️⃣SEMINA YA NENO LA MUNGU UWANJA WA WAJENZI-DODOMA : NA MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE

1️⃣SEMINA YA NENO LA MUNGU UWANJA WA WAJENZI-DODOMA : NA MWL. CHRISTOPHER  MWAKASEGE

SIKU YA KWANZA: 27 APRILI, 2022

SOMO: “MANENO PINGAMIZI YASIKWAMISHE UAMSHO WAKO BINAFSI” 

UTANGULIZI

LENGO YA SOMO

Uamsho kutoka kwa Mungu uliokusudiwa kwa ajili yako uweze kuupata. Na msisitizo hapa haupo kwenye maneno bali upo kwenye uamsho. Na kati ya kitu kimojawapo tutakachoshughulika nacho kwenye somo hili ni maneno pingamizi ambayo yanatafuta kila namna ya kukukwamisha ili usipokee kile Mungu alichokikusudia kwako na usifike pale Mungu alipokusudia ufike.
 
Na kwa leo nataka tujifunze na kuangalia juu ya UMUHIMU WA UHUSIANO WA UAMSHO WAKO WA LEO NA MAFANIKIO YAKO YA KESHO
 
Soma Matendo ya Mitume 12:1-17
Maandiko yanasema kwenye mstari wa 7 kusema “Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi.” Malaika alimwamsha Petro ili apate uamsho wake binafsi akiwa katika mazingira magumu sana ya kukatisha tamaa.
 
Na hata Petro akipiga picha ya mwenzake aliyemtangulia aliyekuwa akiitwa Yakobo alipita kwenye mazingira kama hayo na kuishia kufa. Kwa hiyo yeye jinsi alivyoshikwa alijua kabisa na yeye alipokuwa akielekea si kuzuri maana mazingira aliyokuwa nayo hayakuwa mazuri yalikuwa ni mazingira magumu sana. Lakini Biblia inasema Malaika alienda pale na kumwamsha Petro pekee.
 
Kwa hiyo ni muhimu ufahamau hii ya kwamba Mungu anapopelekea uamsho mahali hakuna uamsho wa kikundi fulani bali atatafuta Petro wa eneo hilo ili kuleta uamsho wake. Maana hata kwa Petro maandiko hayatuambii walikuwa wafungwa wangapi lakini yanatuambia kulikuwa na mfungwa mmoja aliyeitwa Petro ambaye uamsho ulikuwa kwa ajili yake. Kumbuka pia msalaba si kwa ajili ya kikundi bali ni kwa ajili ya mtu mmoja mmoja. Biblia inasema kwa kila aaminiye na si kwa wale waaminio maana yake unathamani wewe binafsi pale msalabani hata kama uko peke yako ambaye ni mchafu unayehitaji msaada hata kama uko peke yako wakati wengine wote hawamtaki Yesu, Yesu angeweza kuja na kufika msalabani kwa ajili yako na angerudi kulichukua kanisa kwa ajili yako.

Kwanini alipeleka uamsho kwa ajili ya leo ya Petro. Kwa sababu kazi ya uamsho ni kuamsha Biblia inasema akampiga ubavuni.

Zipo sababu kama nne hivi zilizofanya Uamsho wa Petro kwa ajili ya leo yake.

SABABU YA KWANZA
KURUDISHA TUMAINI LA LEO YAKE ILI KUAMSHA TUMAINI LA KESHO YAKE

Nuru iliangaza pale chumbani na hii ilitokea baada ya Malaika kuwepo pale. Nuru inasimama badala ya tumaini. Mwanzo 1:1-4 inazungumzia juu ya uumbaji wa Mungu na maandiko yanatuambia katika sura ile ya pili kuwa Dunia haikuwa katika hali nzuri. Ilikuwa na utupu ukiwa na giza na Roho wa Mungu alitulia juu ya maji na kitu cha kwanza Mungu alipotokea akasema kuwe Nuru. 

Maana yake alikuwa anasema kuwe na tumaini katikati ya giza,ukiwa na katikati ya utupu uliokuwepo.

Ukisoma Isaya 60:1-2
Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa BWANA umekuzukia.  Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali BWANA atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako.

Ile kwamba dunia ipo kwenye giza haina maana na wewe uwe ndani ya giza. Mungu anaweza kuweka nuru upande wa kwako tu na upande mwingine wapo gizani. Katika kitabu cha Kutoka unaona  giza likiwa upande Misri na Gosheni kuwa na Nuru kwenye mapigo ambayo Misri ilipigwa.

Kazi ya Nuru ni kutoa giza mahali lilipo na kuweka nuru. Nuru inadhihirisha uwepo wa Mungu mahali pale kwa ajili yake sio kwa ajili ya group (kikundi).

Biblia inatuambia tukauona utukufu wake, utukufu wa mwana pekee atokaye kwa baba amejaa neema na kweli ambaye hapo mwanzo alikuwa neno na neno alikuwa kwa Mungu.

Biblia inasema ndani yake kulikuweko uzima na ule uzima ulikuwa nuru ya ulimwengu na ile Nuru ya watu yang'aa gizani na wala giza halikuiweza.

Petro alipotembelewa na yule malaika kitu cha kwanza ambacho roho ya uamsho ilileta ni kushughulika na giza kwa sababu alikuwa amefunikwa na giza kila eneo. Alifunika na giza kwenye familia yake kwenye utumishi wake maisha yake ya baadae vyote vilikuwa ndani ya giza hakuwa na tumaini.

Kitu cha kwanza Roho ya uamsho inapokuja ndani ya Mtu ni kwa ajili ya kumletea tumaini katika hali aliyonayo ili apate tumaini la kesho yake.

Roho wa uamsho anapokuja hata akikutembelea wewe kitu cha kwanza ni kukufanyia ni kuachilia nuru ya Mungu na kuachilia utukufu wa Mungu maana yake Mungu anajifunua kwako kwa namna ambavyo anatafuta kuondoa giza na kila kitu ambacho ndani yako ambacho kilifanya upoteze tumaini leo na upoteze tumaini kesho na kwa sababu hiyo Mungu anakuletea nuru hiyo leo ili katika nuru hiyo tumaini lako lirudi na tumaini la kesho litarudi pia.

Ya kwanza
Tumaini lako la kesho linajengwa na tumaini lako la leo,

Ya pili
Leo yako inatengeneza kesho yako, kesho yako inategemea leo yako

Ya tatu
Ukivuruga leo yako umevuruga na kesho yako,

Ya nne
Kukwama kwako leo kunakwamisha kesho yako
Petro alikwama pale kwenye leo yake hakuwa tena na kesho yake.

Yeremia 29:11
Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Mpango wa Mungu kwa ajili yako una leo na kesho ukiiopoteza leo yako unapoteza na kesho yako, ukikwamishwa leo na kesho yako inakwama. Kwa sababu maandalizi ya kesho yako yanategemea maandalizi uliyonayo leo. Kesho haiandaliwi kesho, kesho inaandaliwa leo 

Ya Tano
Shetani anakufunga leo ili usipate kesho yako,
atakufunga kwa dhambi, atakufunga kwa magojwa, atakufunga kwenye fikra kwenye ufahamu kwenye mwili na kwenye kila kitu 

Kitu kikubwa sana anachokitafuta sio leo yako bali ni kesho yako. Sasa ili aipate kesho yako lazima afunge leo yako. 

Shetani naye ni msomaji wa maandiko anajua tunatoka utukufu kwenda utukufu, nguvu kwenda nguvu, imani kwenda imani, kwa hiyo kila kitu kwake ni tishio.

Pamoja na hayo yote Mungu akishaona umesongwa namna hiyo kwa kukosa tumaini la kesho yako ataleta roho ya uamsho ili maombi yafanyike kurudisha tumaini lilipotea. Hii ni sawa na hospitalini wakiona mtu kapoteza tumaini la maisha daktari anaweza kumtafuta mshauri au kiongozi wake wa dini au ndugu yake anayeweza kuzungumza naye juu ya tumaini la maisha kwake. Kwani mtu akikosa tumaini la kuishi hakuna faida ya kumpa dawa kwani hazitamsaidia. 

Ili uweze kuendelea kitu cha kwanza Mungu anakurudishia nuru kwanza inayoleta tumaini. 

SABABU YA PILI YA MUNGU KULETA UAMSHO 

KUAMSHA NEEMA NDANI YA MTU YA KUSIKIA NA KUTII MAELEKEZO YA MUNGU LEO ILI AIPATE KESHO YAKE
Ili uweze kuwa na kesho yako sawasawa na Mungu alivyokupatia lazima ufuate maelekezo yake. Baraka za Mungu zipo mwanzoni mwa kutii kwako. 

Watu wengi wanataka Mungu awabariki ndipo wamfuate ila Mungu anataka watu wamfuate halafu baraka zinakuwa sehemu ya maisha yao unapomfuata Kristo. 

Tunatakiwa kumwamini Mungu kwa kutupatia upendo wake pale msalabani. 

Matendo ya Mitume 12:7-8
“Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi. Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate.”

Petro alipigwa ubavuni ili kutukumbusha kile kilichofanyika msalabani kwa kuchomwa mkuki ubavuni na maji na damu vikamtoka. Hii ni sawa na mwanamke anapojifungua, chupa hupasuka na kutoa maji na damu hii huonesha kulinda kilichoko ndani.

Angeweza kumpiga mahali pengine lakini alipompiga kwenye ubavu ilikuwa ni alama kwamba hajamsahau na wala hafanyi kwa kumpendelea bali ni kwa sababu alishika maagano yake ya pale msalabani. 

Haijalishi mahali unapopita, Bwana analikumbuka agano na atakutoa mahali ulipo. Hata kama amesahau matatizo uliyonayo atakumbuka agano alilokufanyia ambayo ni kwa nyakati hizi na kwa wakati huu hata kama giza limetanda uwe na uhakika asubuhi imekaribia. Hata kama umepoteza tumaini, nuru ya Bwana ikuzukie. 

Inawezekana wanadamu wote wamekusahau; Bwana hajakusahau. Hata kama umefungwa gerezani, atakuja huko kukutazama. 

Maandiko yanasema JIFUNGE… Hili neno kwa tafsiri za Kiingereza sio kujifunga tu kama kwa kutumia mkanda maana yake avae mavazi mbalimbali. Yaani aliambiwa ajifunge, avae viatu vyake na akaambiwa afunge nguo zake amfuate Yesu. 

Iko hivi: Petro alifungwa, muda huu ulipofika minyororo ilimtoka. Walipomvua nguo maana yake walimfanyia dhihaka. 

Neno kwenye Luka 10 linasema popote watakapowapokea na amani imo hapo semeni. Neno la namna hii linapotimia maana yake ile heshima uliyopoteza inarudishwa. 

Alipoambiwa avae viatu sio tu viatu hivi vya kimwili bali ni katika ulimwengu wa roho maana yake alivuliwa UTAYARI wa kusonga mbele na maisha pia na utumishi pamoja na mamlaka aliyokuwa nayo ya kukanyaga nyoka na nge, juu ya nguvu za giza. 

Kuna wakati unakemea mapepo hapa na pale na yanatoka ila kuna muda unafika unapoteza hizo nguvu na utayari wako. Hata ukiletewa mwenye mapepo ndani yako unasemeshwa maneno magumu sana na yule mwovu adui kwamba kama umeshindwa ya kwako utawasaidiaje wenzako achana na hiyo. 

Watakusemesha kwenye mawazo yako. Kinachofanyika hapo ni kukuvua viatu vyako. Umeacha hiyo biashara kwa sababu kuna mahali unapita. 

Leo Mungu anakurudia akisema uvae viatu vyako (utayari wako) kwa sababu mbele yako kuna vitu muhimu vya kufanya kwani Mungu amekurudishia mamlaka yako. 

Na viatu unavalia kwenye mazingira hayo hayo wala sio nje na hapo ili wajue ya kwamba utayari unao na Yesu uko naye. 

Yesu aliposema Petro ajifunge nguo yake (koti la juu) hii pia ina maana yake. 

Mfano wakati Eliya anaondoka kwa kuvuka mto Yordani, alimzuia sana Elisha kuwa asimfuate huku amebeba koti lake la juu na akapigia nalo maji nayo yakapasuka wakasonga mbele. Ndipo alipomgeuka Elisha na kumwambia aombe lolote na atapewa. 

Elisha akaomba roho mara dufu. Ilikuwa ngumu lakini akamwambia akimwona anaondoka hiyo roho ataipata. Na wakati anaondoka na gari la moto ndipo akamwachia vazi na akapiga maji nayo yakapasuka. 

Alipovuka ng'ambo wale wana wa manabii wakasema roho ya Eliya iko juu yake. Maandiko yanasema hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa Elisha kurushiwa vazi na Mungu alipoona Eliya alipofika hawezi kuendelea akasema amemchagua Elisha. 

Vazi lilipomshukia Elisha ghafla ndani yake akasikia wito ndipo akaomba kibali ya kurudi nyumbani kuwaaga. Ndipo Elisha akaenda nyumbani na kuchinja ng’ombe sawasawa na neno la Yesu kuwa mtu akimfuata ajikane nafsi yake. Maana yake anaua ubinafsi ndani yake. Sasa lile vazi la juu linasimamama kwa nafasi ya upako, utambulisho wa Mungu kwa watu. 

Mwingine unajifungia ndani hutaki kufanya kazi kumbe bado Mungu anakuhitaji ufanye kazi yake kwa sababu amewekeza kwako kwa ajili ya kesho yako. Kwa hiyo kama umepoteza upako Roho Mtakatifu yupo hapa kukusaidia. 

Kama umekosa utambulisho wa Mungu kwa watu, Bwana anaurejesha. 

Katika habari hii ya Petro tunaona ya kuwa Kanisa liliomba kwa juhudi kwa ajili ya yake (Mdo 12:5). Ukiona mpaka kiongozi akuambie uombe ujue uamsho haujaja ndani yako. Mfano yule nabii mwanamke Anna aling'ang'ana na kuomba kwa unabii wa Yesu kutokea, alikuwa hekaluni peke yake ili hali ilikuwepo ndani na hakuna aliyemlazimisha. 

Roho ya uamsho inaletwa na Mungu na inategewa kwa watu ambao wako tayari kujua alama za nyakati mioyoni mwao na wakaendelea kuomba. Kama watajikusanya wawili, 5, 10 n.k ili waombe. 

Kabla roho ya uamsho kwenda kwa Petro, Mungu alitafuta waombaji kwanza na tunajua hakuna uamsho bila maombi. Tukipoteza utii kwenye maombi tutapoteza roho ya uamsho na tutapoteza akina Petro wengi. 

Biblia inasema fufua kazi yako katikati ya miaka… (Habakuki 3:2) maana yake lazima kwanza kuwe na waombaji. Kwa hiyo kama kuna mtu mmoja Mungu anamtafuta ile roho ya kumwamsha haitaenda kwake kwanza bali kwa (wanamaombi) mwombaji kwanza. 

Maombi haya hayatajalisha muda wala idadi ya waombaji, huyo aliyepewa jukumu la kuomba ataomba hadi aone. Hata kama nuru itaonekana gerezani na haimtoi mtu huko haisaidii. 

Kumbuka kwa Yusufu nuru ikamwangazia gerezani na kuheshimika huko hata kupewa nafasi ya uongozi hata na wewe unaweza ukawa mfungwa wa aina fulani na bado ukabaki gerezani, usitosheke na kukaa hapo. Msalaba wa Yesu Kristo haupo kwa ajili ya kukarabati gereza bali ni kwa ajili ya kukutoa gerezani. 

Mwingine akiona miujiza miwili mitatu anasema tumemwona Mungu akifungua watu na wakaishi hapo uwe na uhakika na Malaika watamwachia njiani. Nguvu za malaika inategemea nguvu za waombaji katika mazingira ya uamsho. 

Unaweza kusema Mwakasege mimi sina hata nguvu za kuomba, mwombe Mungu akuinulie watu wa kuomba kwa ajili yako. Mwambie Mungu "sina nguvu za kuomba, naomba uniinulie watu wa kuniombea nisije nikaozea huku magerezani". 

Hatuoni mahusiano kati ya Petro na wenzake waliomwombea kule. Kwani hata namna ya kumwuliza haikuwepo bali waliingia katika maombi ili atoke. 

Sheria ya vitani iko hivi: kama askari mwenzako akitekwa humwulizi alifanya uzembe gani bali unamwokoa, na kumhudumia ndipo utamwuliza ili mjue nini kilimpata ili nanyi msifanye kosa hilo. Ukiona makosa ya wenzako yakupeleke kwenye magoti - kuomba (kuwasemelea kwa Bwana) siyo kwenye kikao.

Malaika atafuatilia kila kitu wakati ninyi mnaomba kama vile ilivyokuwa kwa Petro kusindikizwa hadi nyumba walimokuwa wanaomba. Maombi yetu mengi tunayaachia njiani ila kama kesho yako na yao ikiunganika mambo yataenda vizuri ila kama hayajaunganika lazima mtavurugika. 

Usitafute roho ya uamsho ikutoe mahali ulipo, tafuta roho ya uamsho ya maombi kwanza kwani ndiyo yatakutoa wewe na wengine. 

Karibu tuombe wote kama unahitaji maombi haya ya uamsho ili kwamba Mungu akikuhitaji saa yoyote aone utayari ndani yako. Roho wa maombi ya uamsho ikishuka hakuna atakayebisha hata kama upo katika mazingira magumu kivipi utatafuta kuomba. Haya kama unauza biashara yako, utajifunza kuomba. 

Kama ni ofisini hawakuelewi utaenda hata chooni kuomba. Ukifika huko utanena kwa lugha na kuomba zaidi kwa sababu hakuna mtu atakayekuuliza kuwa kwanini umechelewa kutoka chooni kwa sababu mambo ya chooni ni siri ya aliyeingia huko. Na waking'ang'ana kukuuliza waambie kazi ilikuwa nzito 😂 😂.
Wimbo - Tenzi Za Rohoni 

23. NI SALAMA ROHONI MWANGU

🎵Nionapo amani kama shwari,
Ama nionapo shida;
Kwa mambo yote umenijulisha,
Ni salama rohoni mwangu.

    🎶Salama rohoni,
    Ni salama rohoni mwangu.🎶

🎵Ingawa shetani atanitesa,
Nitajipa moyo kwani
Kristo ameona unyonge wangu,
Amekufa kwa roho yangu.

🎵Dhambi zangu zote, wala si nusu,
Zimewekwa msalabani;
Wala sichukui laana yake,
Ni salama rohoni mwangu.

🎵Ee Bwana himiza siku ya kuja,
Panda itakapolia;
Utakaposhuka sitaogopa
Ni salama rohoni mwangu.

*🎶🎵It Is Well With My Soul 🎵🎶*

Fuatilia maombi ya Somo hili YouTube kupitia link pale juu. 

Ubarikiwe Sana. Tukutane siku ya pili ya semina hii.

Comments

Popular posts from this blog

TISS YAPATA BOSS MPYA.

  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, Amemteua Bw.Said Hussein Masoro kuwa Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa taifa,Kuchukua nafasi ya Kamishina Diwani Athuman Msuya  Ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Kabla ya Uteuzi huo Bw.Masoro alikua akihudumu katika Idara ya Usalama wa Taifa kama Naibu Mkurugenzi mkuu na Mkurugenzi wa shughuli za  ndani wa Usalama wa Taifa. Wakati huo huo Rais Dkt.Samia amemteua Balozi Hussein Othman Katanga Kuwa Balozi wa Tanzania mjini New York, Nchini Marekani na muwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa. Balozi Katanga anachukia nafasi ya Balozi Profesa Kennedy Gaston,Ambaye Uteuzi wake umetenguliwa. Balozi Katanga kabla ya Uteuzi huu alikua Katibu Mkuu Kiongozi. Vile vile Mhe.Rais Dkt.Samia amemteua Bw.Moses Mpogole Kusiluka Kuwa Katibu Mkuu Kiongozi,Ambapo kabla ya Uteuzi huo alikua Katibu Mkuu Ikulu. Taarifa Rasimi Kutoka Kurugenzi ya mawasiliano ya Raisi Ikulu iliyotolewa mapema Jana Januari 3,2023, i...

JESHI LA POLISI LATANGAZA AJIRA KWA MWAKA 2012/2013 KWA WAHITIMU WATARAJIWA WA VYUO

TANGAZO LA AJIRA Jeshi la Polisi Tanzania katika mwaka wa fedha 2013/2014 litaajiri vijana kutoka katika makundi yafuatayo: waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012, kidato cha sita mwaka 2013, JKT/JKU mwaka 2013 na vyuo vya elimu ya juu mwaka 2013. Taratibu zinakamilishwa ili waliomaliza kidato cha nne na sita na waliojaza fomu za maombi kabla ya kumaliza mitihani yao ya mwisho waitwe kwenye usaili. Usaili wa vijana wa JKT umekamilika mapema mwezi Aprili, 2013. Tangazo hili linawaalika vijana walioko kwenye vyuo vya elimu ya juu nchini watakaohitimu masomo hivi karibuni na wanaopenda kujiunga na Jeshi la Polisi kujaza fomu za maombi zinazopatikana kwenye tovuti ya Polisi kwa anuani www.policeforce.go.tz www.policeforce.go.tz Fomu za waombaji baada ya kujazwa kikamilifu ziletwe na mkuu wa chuo kabla ya tarehe 30/6/2013 kwa: Inspekta Jenerali wa Polisi, Makao Makuu ya Polisi, S.L.P. 9141, DAR ES SALAAM . Fani zinazotakiwa ni; Shahada za Menejimenti ...

GET TO KNOW EXTENDED MARKERTING MIX

The extended marketing mix is, as the name suggests, an extension of the marketing mix which was traditionally for products. The 4P’s are also known as product marketing mix. As services came more into the picture it was seen that the 4p’s could not justify the marketing mix. There were 3 more elements which were necessary to actually explain the marketing of services. When products began offering services, the extended marketing mix began applying to products as well (like Maruti service stations where Maruti is a product and the service station is a service). These are the elements which were added to the marketing mix to form the extended marketing mix. In the above figure, the product marketing mix are the first four P’s and the next 3 P’s are added to make the Extended Marketing mix. This extended marketing mix is also known as the service marketing mix. The four PS mainly constituted the following 4 elements Product Price Place Prom...