SHALOM WAPENDWA
Leo nataka tujifumze Juu ya SADAKA hii ya Miili yetu,Maana Tumejifunza Juu ya matoleo mbalimbali Kama Fungu la kumi, SADAKA ya Shukrani,Kusaidia wasiojiweza Ndani ya KANISA Lakini ni Nadra Sana kufundishwa SADAKA ya Mwili wa Mwamini....
Meno La Tafakari Ni *WARUMI 12:1*
*1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.*
Hivi Mimi na wewe TUNAITOA KIKAMILIFU Ili TUWEZE kumfanyia Mungu Ibada Yenye Maana?
Natukumbuke SADAKA zote Ili zitimize Ibada Yenye Maana huenda pamoja,Tunatoa labda Fungu la Kumi/zaka KWA uaminifu Sawa Lakini Miili yetu nayo tumeitoa kikamilifu❓❓
VIP hapo tuna Ibada Yenye Maana❓Au tumepoteza Muda Wetu Na SADAKA imekataliwa...🤔🤔
Kristo msingi was Imani yetu yeye akitufundisha KWA kuutoa Mwili wake usulubiwe na ikawa SADAKA /Dhabihu Yenye kupendeza Ambayo hakuna Mwanadamu Mwingine Awaye Yeyote ameitoa SADAKA ya Namna hiyo.
Ndipo Mtume Paulo Naye anatukumbusha Kuwa ...... Tuvifishe viumgo vyetu vilivyo Katika nchi Ili tufanye Ibada ya maana
*Kolosai 3:5* *Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;*
Sasa He Miili yetu Ni SADAKA kamili?? au nayo Imekua Ni wizi Kama tunavyo iba Zaka?? Miili yetu tunaifujaaa kwenye mapombe,Zinaa uasherati,UONGO wizi Rushwa masengeng'enyo Harafu tuna beba na Zaka pungufu Tunasongeza madhabahuni pa BWANA GHADHABU ya Mungu Inayo Kuja tungeiona Kheri Tughaili Mabaya Haya Tutubu Na Tutengeneze Upya Tuiepuke.
Eeeh Mungu Ingilia Kati Juu ya Hili 😭😭😭😭😭 *Nawatakia Tafakari njema*
Comments
Post a Comment