Shalom Kanisa👋
Wapendwa leo Tutafakari juu ya Mawazo Yetu Wenyewe ndani ya Mioyo Yetu,Hebutusome hapa Yeremia 4:14 NENO linatufundisha
Ee Yerusalemu, jioshe moyo wako usiwe na uovu, upate kuokoka. Mawazo yako mabaya yatakaa ndani yako hata lini?
Mawazo mabaya TUNAYO jiwazia Wenyewe na Kisha kuwawazia wengine yatakaa ndani ya Mioyo Yetu Hata lini???
NENO latufundisha tujitakase TUSIWE na Uovu,Mwisho Yale tujiwaziayo mabaya yatoke ndani ya Mioyo Yetu, Tupo leo WATU tunawaza je nikifa? ntazikwaje,Wanangu wakifa ntakua nahali Gani Mme/MKE akifa nitaishije? Nasafiri nikipata Ajali je? Ukiona una Mawazo ya Namna hii kongwa la ashetani limekuatamia leo pona Mteule, Shetani hutumia mwanya huo Wa Mawazo mabaya tujiwaziayo Wenyewe Kutu weka Tanzini.
Ikiwa Mungu atuwazia yaliyo mema kwanini sisi Watoto wake tujiwazie mabaya❓❓🤔 Hebu tujifunze KWA kusoma Hapa Yeremia 29:11 .....Enhee nambie Mteule umejifunza nini KATIKa Aya hiyo❓Ikiwa Mungu akuwazia hivyo Kwanini wewe ujiwazie kinyume chake❓Hapo jipime uko Upande Gani Wa Mungu au Wa Yule nyoka wa zamani❓
Kumbe Wapenzi tumeelekezwa na NENO Kuwa Tutafakari Mambo Yaliyo mema na mazuri KWA Utukufu Wa Mungu Filip 4:8
Lakini Kumbe NENO litufundishapo kulinda Sana Mioyo Yetu Maana huko Ndipo zilipo chemchem za uzima hututakaa Tujiwazie Wenyewe na wengine Mambo Yaliyo mema, Mithali 4:23
Karibuni Tutafakari Wapendwa.
Comments
Post a Comment