Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa Kigoma,Ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mkoa Kigoma Bw.Malima Mobutu, imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani Kakonko,leo Juni 30,2023. Katika ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi, Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mesha Mallasa,ameambatana na Kamati ya Usalama Wilaya Kakonko, Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya Kakonko pamoja na wakuu wa idara mbali mbali kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya Kakonko. Akizungumza Wakati wa Majumuisho ya ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Mkoa Kigoma Bw.Mobutu ameeleza namna Kamati ya siasa ilivyoridhishwa na namna miradi hiyo inavyoendelea kutekelezwa Wilayani Kakonko,na amewataka watendaji kurekebisha kasoro ndogo ndogo zilizo bainika katika Miradi iliyotembelewa na miradi mingine Yote inayoendelea kutekelezwa. "Kwa niaba ya Kamati ya siasa ya Chama,nitumie Fursa hii kuwapongeza watendaji wote,na kwa ujumla nis...