Skip to main content

MKUU WA WILAYA KAKONKO AWATAKA VIJANA KUZINGATIA MAADILI.

 Na. A.C KUZENZA 

Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mallasa,amewaasa vijana Wilayani Kakonko kuzingatia maadili mema yenye kulinda utu wa mtu na kuzingatia maadili ya kiafrika hususani yale ya Kitanzania.



Ametoka Wito huo  Leo Ijumaa Aprili 21,2023 wakati wa Sherehe za Mahafali ya 1 ya Chuo Cha Elimu ya Ufundi Stadi JKT Kasanda, kilichopo Wilayani  Kakonko mkoani kigoma.  

Akiwahutubia wahitimu hao,Kanali Mallasa,amewataka vijana hao kuyatumia mafunzo waliyoyapata chuoni hapo kutumia fursa  za miradi inayotekekezwa Wilayani Kakonko kupunguza Uhaba wa mafundi katika Fani mbali mbali jambo linalopelekea Wilaya kutafuta Mafundi Kutoka nje ya Wilaya  jambo linalo pelekea kudumaza Uchumi wa Watu wa Kakonko.

"Wilaya ya Kakonko tunao uhitaji mkubwa wa mafundi  wa fani mbalimbali,hali inayopelekea kutafuta mafundi kutoka nje ya Wilaya yetu,Kwa uwepo wa chuo hiki naiona changamoto hii inakwenda kupungua" Alisema Kanali Mallasa

Aidha Amewasisitiza wahitimu hao Kuwa waaminifu katika maeneo yao ya kazi na kuweka mbele Uzalendo Kwa Nchi yao, na kuto kubweteka na ngazi hiyo ya mafunzo waliyoipata.

"Pamoja na kupata mafunzo katika Fani mbalimbali msibweteke na kuishia hapa jiendelezeni,huku mkiendelea Kuwa wazalendo,..Wilaya yetu inahitaji mafundi waadilifu na wazalendo" alisisitiza Kanali Mallasa.

Wakisoma risala Yao Mbele ya Mgeni Rasimi,Wahitimu wameainisha Changamoto zinazo wakabili Wanafunzi wakati wa mafunzo,  Kubwa ni uhaba wa vifaa vya kujifunza hasa kwa vitendo Jambo linalopelekea kushindwa kujifunza kwa vitendo kwa muda wa kutosha.



Naye Mkurugenzi wa Mafunzo Stadi Kutoka Jeshi la Kujenga Taifa, Luteni Kanali,Thobias Jackson Ngailo amewatka wahitimu hao wakafanye kazi kwa weledi na Maadili Ili wawe mfano mzuri katika Jamii ukizingatia chuo walichopata mafunzo ni chuo Kilicho Chini ya Jeshi la Kujenga Taifa.

"Vyeti mlivyovipata leo ni kipande tu cha karatasi,tunategemea mkafanye kazi kwa kuzingatia maadili kulingana na taaluma zenu" amesisitiza Luteni Kanali Ngailo

Vile vile Luteni Kanali Ngailo,ameahidi Kuwa  Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa itaendelea kukiongezea Uwezo chuo hicho kwa Kuongeza nyenzo za kufundishia hasa mafunzo kwa vitendo.

"Tunategemea kukiongezea  chuo Nyenzo za kufundishia kwa vitendo katika fani za Uchomeleaji,Udereva Ufundi Magari (Mechanics Engineering) na kozi zingine" ameongeza Luteni Kanali Ngailo.



Naye Mkuu wa chuo Cha Mafunzo ya Ufundi Stadi JKT Kasanda, Meja Benedicto Lubida,akisoma taarifa ya Chuo Mbele ya mgeni rasimi,Mkuu wa Wilaya Kakonko Kanali Evance Mallasa ameeleza Chuo Cha JKT Kasanda kinatoa Mafunzo ya Ufundi Stadi katika Fani za,Udereva,Uchomeleaji,Umeme wa majumbani,Kompyuta,Saloon na urembo,Upishi Pamoja na ushonaji  kwa kozi za mda mfupi na za mda mrefu kwa ngazi 1,2 na 3.



Aidha katika mahafali  hayo jumla ya Wanafunzi 22 kati yao Wanawake ni 7 na wanaume ni 15 wamehitimu mafunzo  ngazi ya 3 katika fani tofauti,ambapo Udereva wamehitimu Wanafunzi 12,Saluni na mapambo Wanafunzi 4,na Kompyuta Wanafunzi 6.


Comments

Popular posts from this blog

MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE.

 “MANENO PINGAMIZI YASIKWAMISHE UAMSHO WAKO BINAFSI” (2) Siku ya Pili 28, Aprili 2022  Semina ya Neno la Mungu - Dodoma LINK YA SOMO LA HILI YOUTUBE 👉🏼 https://youtu.be/Rwo70MEHQd0    NAMBA ZA KUTUMA SADAKA, MAOMBI NA SHUHUDA 👉🏼https://bit.ly/Sadaka-Maombi-Shuhuda  UTANGULIZI LENGO YA SOMO ➖Uamsho kutoka kwa Mungu uliokusudiwa kwa ajili yako uweze kuupata majira haya nyakati hizi. Wasomaji wa Biblia, historia ya ulimwengu na kanisa wanajua kabisa kipindi chochote kinachotangulia matatizo, kinachofuata ni maombi na baadaye unafuata uamsho. Kama kuna tatizo limepita katika taifa, ujue kuwa kuna watu watainuka kuomba kwa ajili ya lile taifa, na matokeo yake ni uamsho katika lile taifa. Hili lipo katika kanisa, familia na mahali pengine popote. Msisitizo wa somo hili ni ujue namna ya kufanya wakati Mungu anaachilia uamsho huu katika nyakati hizi, maneno pingamizi yasiwe kikwazo kwako. Pia ujue kitu cha kufanya katika kupokea uamsho huu. Uamsho unaanza na mtu bin...

7 BUSINESS LOCATION THAT INCREASE BRAND VISIBILITY

Marketing has changed and it has become more personal. People nowadays need convenience and you cannot expect that your customer will come to you. You will have to go to your customer again and again so that he does not switch to any other brand. Remember that your customer has numerous options in his hand. Thus your business needs to present in locations where the customer can make his buying decision easily. This is where your business location plays an important role. The process of managing a business is continually changing but more importantly with the advent of online marketing, your business location itself has changed. Because of the increasing usage of internet, Smart phones too are the latest trend and hence the reach of internet is now quadrupled. But it is not necessary that your customer be present only on the internet. Brick businesses are as alive today as online businesses. Below you will find a list of 7 business locations that you should be ...

GET TO KNOW EXTENDED MARKERTING MIX

The extended marketing mix is, as the name suggests, an extension of the marketing mix which was traditionally for products. The 4P’s are also known as product marketing mix. As services came more into the picture it was seen that the 4p’s could not justify the marketing mix. There were 3 more elements which were necessary to actually explain the marketing of services. When products began offering services, the extended marketing mix began applying to products as well (like Maruti service stations where Maruti is a product and the service station is a service). These are the elements which were added to the marketing mix to form the extended marketing mix. In the above figure, the product marketing mix are the first four P’s and the next 3 P’s are added to make the Extended Marketing mix. This extended marketing mix is also known as the service marketing mix. The four PS mainly constituted the following 4 elements Product Price Place Prom...